BancABC Tanzania ambayo ni kampuni tanzu ya Atlas Mara leo imetangaza kuzindua kampeni kabambe ya kuweka fedha katika akaunti ya amana (fixed deposit) kwa wateja wote, ambapo kwa sasa mteja ataweza kupata riba ya hadi asilimia 14 kwa mwaka.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza kampeni hiyo, Muendeshaji Mkuu wa Biashara wa BancABC Tanzania Joyce Malai amesema kuwa benki hiyo imeanzisha utaratibu wa kutoa riba ya hadi asilimia 14 kwa wateja wote wanaofungua akaunti za amana kuanzia leo mpaka mwishoni mwa mwezi Septemba na mteja atalipwa riba hiyo papo hapo huku fedha ikiendelea kusalia kwenye akaunti mpaka pale itapofikia muda wake uliokusudiwa (mwaka, miezi sita au miezi mitatu).

‘Hii ndio ofa kabambe na bora kwenye soko kwa sasa, kwa hiyo nachukua nafasi hii kuwahimiza wateja wetu na pia kwa wale ambao sio wateja wetu kuchangamkia fursa hii na kuwekeza kwenye akaunti ya amana ya BancABC kabla muda wa ofa hii haujaisha’, Malai alisema.

Malai alisema kuwa BancABC imedhamiria kuendelea kutimiza mahitaji ya wateja wake kwa kuhakikisha kuwa wote wanafaidika na wanakuwa kwa pamoja. Tunatoa riba papo hapo ili kufanya wateja wetu waendelee kuendesha biashara zao pamoja na shughuli zao za kila siku bila kusubiri muda wa uliokusudiwa wa akaunti ya amana ufike ndio wapate fedha zao. Hili la BancABC kutoa malipo ya riba mwanzoni ni jibu la ombi lililotolewa na wateja ikiwa ni hatua ya kufaidi mapema pato au mavuno yanayotokana na uwezekezaji wao kwa kipindi hicho.

‘Vile vile, tumetoa uhuru kwa mteja anayetaka kuchukua riba yake baada ya robo ya mwaka, nusu ya mwaka au hata baada ya mwaka ikiwa hataki kuchukua punde tu anapowekeza. Kwetu sisi BancABC, mteja ni mfalme na ndio sababu tumetoa uhuru huu ili kukidhi mahitaji ya wateja wetu wote’, alisema Malai.

Akizugumzia zaidi juu ya kampeni hii, kaimu mkuu wa kitengo cha Haina Luiza Paschal, aliongeza kuwa mteja anaweza kukopa kutokana na amana ya akaunti yake iwapo atahitaji mkopo. Tunaomba wateja wetu wote watumie fursa hii kabla ya muda wa ofa kuisha.

‘Unachotakiwa kufanya ni kupiga namba 0779 111 000 au tembelea matawi yetu yaliyopo Dar es Salaam (Uhuru, Tegeta na Kariakoo), Dodoma, Arusha na Mwanza, fungua akaunti ya amana kisha upate riba yako papo hapo’, Malai alisema.

Ofa hii ni kwa wateja wanaofungua akaunti ya amana na BancABC Tanzania kwa mwaka mmoja kabla ya tarehe 30 Septemba 2021.
Muendeshaji Mkuu wa Biashara wa BancABC Tanzania Joyce Malai akizungumza leo jijini Dar es Salaam baada ya benki hiyo kuzindua kampeni kabambe ya kuweka fedha katika akaunti ya amana (fixed deposit) kwa wateja wote, ambapo kwa sasa mteja ataweza kupata riba ya hadi asilimia 14 kwa mwaka. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Hazina wa benki hiyo Luiza Paschal.
Muendeshaji Mkuu wa Biashara wa BancABC Tanzania Joyce Malai (kulia) na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Hazina wa benki hiyo Luiza Paschal wakionyesha bango baada ya benki hiyo kuzindua kampeni kabambe ya kuweka fedha katika akaunti ya amana (fixed deposit) kwa wateja wote, ambapo kwa sasa mteja ataweza kupata riba ya hadi asilimia 14 kwa mwaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...