CHAMA Cha Mapinduzi(CCM),Mkoa wa Dar es Salaam, kemewaita  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Siporah Liana na Meya wa Manispaa hiyo Songoro Mnyonge kufuatia  kutupiana maneno  wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani, hivi karibuni.

Katibu wa CCM wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shaibu  Akwilombe, amesema Kamati ya Siasa ya  Chama, Mkoa, itawata kesho  na kuwahoji  Meya na Mkurugenzi ambapo pia Mkuu wa Mkoa  huo Amos Makala aitashiriki.

“CCM hairidhishwi na  uhusiano baina ya awatendaji wa halmashauri na Baraza la Madiwani  la Manispaa  ya Kinoni,”alisema Akwilombe.

Ameyasema hayo wakati wa kuhitimisha ziara ya Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, kukagua miradi ya maendeleo ya Chama na ya Serikali katika Wilaya ya Kinondoni.

Akwilombe alisema,  licha ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Amos Makala kujaribu kuingilia kati sakata hilo lakini Chama kitaita pande zote ambazo ni baraza la madiwani na  halmashauri ya manispaa, ili kujua kiini cha uhusiano huo mbovu na kutoa maelekezo .

Alisema katika suala hilo CCM itachukua hatua stahiki kwa wahusika.

” Uhusiano huo mbovu uliopo katika  Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni,  umeanza kuathiri maendeleo ya halmashauri hiyo jambo ambslo linakwamisha utekelezaji wa Ilani ya Chama,”alibainisha Akwilombe.

“Tumeambiwa hivi sasa kuna ukaguzi maalumu wa hesabu unaendelea  katika halmashauri.Hii ikifanyika inathibitisha kuwa katika manispaa ya Kinondoni hawaaminiani na miradi itasimama tu ili kupisha ukaguzi huo.Hatuewezi kwenda hivyo”alisema  Katibu huyo wa Chama,”Katibu huyo  wa Chama.

Akwilombe alibaendelea kusema,  mgogoro huo unaathiri utekelezaji wa Ilani ya CCM hivyo  hawatasita  kuchukua hatua stahiki ili halmashauri hiyo iwatumikie wananchi kwa maslahi ya Taifa.

“Katika uongozi hakuna jambo baya kama kuona wote walio kutangulia walikuwa hawafai.Ieleweke kuwa sisi wote ni binadamu na kila binadamu anamapungufu yake,”alieleza Katibu huyo.

Mjumbe wa  Hakmshauri Kuu ya CCM (NEC) Yusuf Nasoro,alisema mgogoro huo wa kiutendaji katika Manispaa hiyo haukubariki na Chama kitachukua hatua.

“Kamati ya Siasa ya Mkoa imewaita   na tutawahoji ili kujua nini kinaendelea katika halmashauri hii.Chama hakijafurahishwa na hali hii”alisema   Nasoro.

Hivi karibuni wakati wa kikao cha baraza la madiwani katika halmashauri hiyo yaliibuka majibizano makali baina ya Mkurugenzi  Sipora na Meya Mnyonge  ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Makala alilazimika Kuwaita na kujaribu kiwasuluhisha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...