
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akimueleza jambo Naibu waziri wa Ujenzi na uchukuzi Mwita Waitara wakati alipotembelea uwanja wa ndege wa Nduli uliopo mkoa Iringa kwa ajili ya ujenzi wa uwanja huo.


Na Fredy Mgunda,Iringa.
MKUU wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amemuomba naibu waziri wa ujenzi na uchukuzi kuhakikisha wakandarasi wanaojenga uwanja wa ndege wa Nduli wanalipwa fedha kwa wakati ili kuhakikisha ifikapo mwezi wa kumi na mbili unakuwa umekamilika na wananchi wanaanza kuutumia katika kipindi cha krismass.
akizungumza wakati wa ziara ya naibu waziri wa ujenzi na uchukuzi Mwita Waitara,mkuu wa wilaya alisema kuwa wananchi wa Iringa wanashauku kubwa ya kuutumia uwanja huu katika shughuli za kiuchumi.
alisema kuwa uwanja wa ndege wa Nduli umekuwa na umuhimu mkubwa katika kukuza uchumi wa wananchi wa mkoa wa Iringa kwa kusafirisha mazao ya kilimo kama vile parachichi kupeleka nje ya nchi na mikoa mingine.
kasesela alisema kuwa wananchi wa mkoa wa Iringa wanajituma vilivyo kwenye kilimo cha mazao ya kibiashara ambayo yamekuwa yanachangia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi na kuleta maendeleo kwa mwananchi mmoja mmoja na mkoa kwa ujumla.
alisema kuwa uwanja huo unatakiwa kuanza kufanya kazi katika kipindi cha krismass kwa kuziunganisha awamu zote mbili ziwe kwenye awamu moja kwa kuufunga kabisa uwanja huu na kuufungua uwanja wa ndege wa Ifunda kwa kipindi hiki cha ujenzi.
kasesela alimuomba naibu waziri kuhakikisha analipwa fedha za ujenzi anazotakiwa kwa wakati ili asikwame kwenye ujenzi wa uwanja huo kwa wakati na wananchi waanze kuutumia mapema kwa shughuli za kiuchumi.
uwanja huu kwetu ni muhimu sana sana hasa kwenye kipindi hiki ambacho tupo kwenye uchumi wa kati Iringa tunasafirisha sana mazao ya kilimo kama vile parachichi na mboga mboga kupeleka nje ya nchi.
Kwa upande wake naibu waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mwita Waitara alisema kuwa wamelipokea swala la kulipa kwa wakati wakandarasi fedha ambazo wanazidai ili kuharakisha kwa ujenzi wa uwanja huo ambao unategemewa na wananchi wa mkoa wa Iringa kukuza uchumi wao.
Alisema kuwa watamliapa fedha kwa wakati ili waangalie kama kweli atafanya kazi kwa wakati kama ambavyo amekuwa akidai fedha hizo kwa mara kwa mara kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa uwanja huo.
Mh:Waitara alisema kuwa hata wakandarasi walisema kuwa wapo tayari kufanya kazi kwa awamu moja tu cha masingi kinachotakiwa kumlipa malipo yake kwa wakati ili ifikapo mwezi wa kumi na mbili uanze kutumika.
Waitara alimalizia kwa kusema kuwa uwanja huo wa ndege ukikamilika kwa wakati utachochea kukuza kwa haraka uchumi wa wananchi wa mkoa wa Iringa na kuleta maendeleo kwa kasi ambayo inatarajiwa na wananchi wengi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...