Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
BAADA ya kukosa Tuzo ya Msanii bora wa Kimataifa 'BEST INTERNATIONAL ACT' usiku wa kuamkia leo, Mwanamuziki kutoka nchini Tanzania, Nassib Abdul maarufu kama Diamond Platnumz amewashukuru Watanzania waliomuunga mkono kwa kipindi chote alichokuwa anawania Tuzo hiyo ya Kimataifa.

Kupitia Kurasa zake za Mitandao ya Kijamii, Diamond Platnumz amesema anajivunia umoja wa Watanzania, upendo na uthamini wa vya nyumbani, pamoja na upendo mkubwa ulioneshwa kwake katika kipindi chote hadi siku ya kuwania Tuzo hiyo.

Diamond amesema ni faraja kwa Tanzania kutajwa duniani kuwa na Wanamuziki bora, amesema wakati mwingine Tuzo hiyo inaweza kuja kwa Watanzania, amewaasa Watanzania kuwaunga mkono Wasanii wengine nchini ili kufanikisha azma ya kuleta Tuzo hiyo (BET Award) nyumbani.

“Kupitia tuzo hii nimeona ni kiasi gani watanzania tuna umoja, upendo na kuthamini vya kwetu...Nawashkuru sana kila mmoja wenu kwa Upendo mkubwa mlionionesha...Nifaraja kuona Dunia inapotaja nchi zenye Wanamuziki bora Tanzania inatajwa, ni jambo la Kumshukuru Mungu....Na naamini wakati mwingine Tutaibeba...nitafarijika kesho na kesho kutwa msanii mwingine pia akiwa katika jambo la kuwakilisha Taifa tumpe nguvu kama mlionipa.... sis ni #SwahiliNation sisi ni Taifa la Waswahili”, amendika Diamond.

Sherehe za utoaji Tuzo hiyo zilifanyika Los Angeles nchini Marekani ambapo Msanii kutoka Nigeria, Burna Boy aliibuka kidedea kwa kunyakua Tuzo hiyo ya Kimataifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...