NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

 

 MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambaye pia ni Rais mstaafu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo Juni 19,2021 ameongoza Kikao Maalumu cha Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar.

 

Kikao hicho cha siku moja kimeanza majira ya saa 4:00 asubuhi katika Ukumbi wa Mikutano wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar na kuhudhuriwa na Wajumbe wa Kamati Maalum ya NEC CCM Taifa Zanzibar.

 

Pamoja na mambo mengine kikao hicho kimepokea na kujadili Taarifa ya WanaCCM wanaomba kugombea nafasi ya Ubunge katika Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Konde,Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Kikao hicho pia kimepokea na kujadili Taarifa ya ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi aliyoifanya katika Mikoa Sita ya CCM Kichama.

Kikao hicho cha kawaida kimefanyika kwa mujibu wa Katiba ya CCM ya mwaka 1977 toleo la mwaka 2017 ibara ya 109 (1),(2), (3)(4),(5),(6) (a) -(d).


Makamu Mwenyekiti huyo Dkt. Shein, amewataka Wajumbe kuendelea kufanya kazi za Chama Cha Mapinduzi kwa bidii ili kuhakikisha Chama kinaimarika zaidi.


Kupitia Kikao hicho Dk.Shein ameelezea kuridhishwa kwake na kasi ya Utendaji ya Rais wa sasa Dk.Hussein Ali Mwinyi na kumsihi aendelee kufanya kuchapa kazi na kuhakikisha anatekeleza kwa ufanisi ahadi alizowaahidi wananchi katika kampeni za uchaguzi uliopita.

 

Akizungumza katika Kikao hicho Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, alisema kuwa kazi kubwa iliyopo mbele yake ni kuhakikisha mambo mengi yaliyoainishwa katika Bajeti ya mwaka wa fedha 2021/2022 yanatekelezwa kwa wakati mwafaka.

 

Aliwambia wajumbe hao kwamba Bajeti hiyo imebeba mahitaji muhimu ya makundi yote katika jamii hivyo wananchi watarajie kupata huduma bora za kijamii,kiuchumi na kimaendeleo.

 

Alieleza kuwa Serikali inajipanga kuanza ujenzi wa Barabara za ndani kwa urefu wa umbali wa kilomita 220 pamoja na barabara Kuu kwa urefu wa umbali wa kilomita 200 kwa Unguja na Pemba ili kuwarahisishia wananchi huduma za usafiri.

 

“Tumejipanga vizuri katika kutatua changamoto  za upungufu wa maji,kujenga na kukarabati barabara za ndani na kuu pamoja na kuimarisha huduma za Afya”,alieleza Dk.Hussein.

 Kwa upande wa wajumbe wa Kikao hicho wamempongeza Rais wa Zanzibar Dk.Hussen kwa kufanya ziara yake ya Kichama iliyowapa matumaini makubwa wananchi juu ya mikakati mizuri ya utekelezaji mipango ya maendeleo nchini.

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambaye pia ni Rais mstaafu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiongoza Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar, kilichofanyika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...