Bolt – Mfumo wa kuagiza usafiri kupitia mtandao ndio mojawapo ya mifumo ya usafiri inayotumiwa sana nchini, kutokana na urahisi, unafuu na usalama wake.
Kama jukwaa linalokua kwa kasi zaidi la upatikanaji wa usafiri kupitia mtandaoni barani Afrika, Bolt hutoa vidokezo na taarifa za kwa abiria ambazo zitawafanya wasafiri kwa usalama kwa urahisi kabisa kupitia vidole tu.
Nchini Tanzania, Bolt inapatikana katika miji ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Dodoma ambapo inakupatia huduma nzuri na kwa bei nafuu zaidi.
Zifuatazo ni dondoo 5 ambazo zinakuwezesha wewe mtumiaji wa Bolt kufurahia huduma zetu kwa usalama zaidi.
1. Agiza usafiri na umsubiri dereva ukiwa katika sehemu salama – Unapoagiza usafiri, hakikisha upo katika sehemu salama. Huna sababu ya kutumia muda mrefu kusubiri usafiri huku ukiwa umesimama nje na simu yako mkononi. Bolt inakuonesha wakati dereva anawasili kwa hiyo subiri ndani hadi dereva atakapowasili. Kwa njia hii unakuwa salama zaidi hadi dereva wako atakapowasili.
2. Hakiki taarifa za aina ya gari na namba zake za usajili – Unapounganishwa na usafiri, unapokea ujumbe wenye taarifa kuhusu jina la dereva, aina ya gari na namba zake za usajili. Hakikisha kuwa taarifa za gari linalokuja kukuchukua zinafanana na taarifa uliyopokea katika simu yako ya mkononi. Ikiwa taarifa hizi haziendani, tafadhali usiingie kwenye gari. Toa taarifa kwa Bolt kupitia kitufe cha huduma kwa wateja kwenye app yako.
3. Vaa mkanda – Daima vaa mkanda! Haijalishi ikiwa umekaa katika kiti cha mbele au nyuma. Pia hakikisha kuwa huning’inizi mikono dirishani na kuwa viungo vyote vya mwili vinabaki ndani ya gari muda wote ambapo gari linatembea. Kuwa mtulivu hadi utakapowasili pale unapokwenda.
4. Wahusishe wapendwa wako: Wape ETA yako: Katika kujali usalama wako, tuna mfumo wa Share My ETA ambao unapatikana katika app yako chini ya taarifa za dereva. Unaweza kutumia mfumo huu kutoa taarifa za safari yako kwa watu unaowaamini kila mara unaposafiri. Mfumo huu unawawezesha wapendwa wako kufuatilia safari yako hatua kwa hatua hadi unapowasili pale unapokwenda.
5. Endapo abiria watataka kutoa taarifa ya tukio, wanaweza kufanya hivyo kupitia app support ya Bolt kwenye simu na pia kupitia barua pepe kwa tanzania@bolt.eu
Ikifanya kazi katika miji zaidi ya 60 ya Kiafrika katika nchi saba, Bolt inapanua na inaboresha huduma zake ili kukidhi mahitaji ya wateja kote barani.
Wakati wowote unahitaji kusafiri au kuzunguka mjini, Bolt iko kwajili yako wakati wowote.
Jisikie huru kutumia vidokezo hapo juu kila wakati unapotumia Bolt.
Kaa salama na ufurahie safari yako.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...