Katibu Mkuu wa Chama  Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo akiambatana na katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi Ndg. Shaka Hamdu Shaka na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Ngemela Lubinga leo wameanza ziara ya siku nne Mkoani Tanga.

Msafara wa Katibu Mkuu ukiwa njiani kuelekea Tanga umesimamishwa na umati  wa wanachama na wananchi kwa ujumla katika maeneo mbalimbali. Katika eneo la Mkata wilayani Handeni katika salamu, Katibu Mkuu  ameeleza kuwa, ziara hiyo imelenga katika utatuzi wa chabgamoto za watu wote baada ya CCM kupata imani kubwa mwaka 2020.

"Tumekuja kushughulika na maendeleo na kutatua changamoto zenu, na hatutakuwa na maneno mengi. Kazi ya Chama chetu ilikuwa kuandaa Ilani na kuinadi mwaka 2020, Kazi tulikamilisha vizuri mkatupa ridhaa ya kuongoza nchi kwa miaka mitano,  kazi yetu sasa ni kusimamia kile tulichoahidi tuone matokeo yake." Ameeleza Katibu Mkuu.

Ziara hii ni ya kwanza kwa Katibu Mkuu na Sekretarieti Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa, ikiwa ni mkakati wa kwenda  mashinani kujenga na kuimarisha Chama.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...