Akizungumza na waandishi wa habari, Kivule, Dar es Salaam, jana, Mkurugenzi wa kituo hicho, Mohamed Mgonza, alisema lengo la kuanzisha kituo hicho ni kutoa fursa kwa vijana wa Kivule, kushiriki katika suala la michezo yote.

"Mji wa Kivule wengi wetu ni tumehamia kutoka maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam, ndiyo maana mimi na wadau wa michezo tumeamua kushirikiana kufungua kituo hichi ili kila mdau wa michezo aweze kuja kushiriki nasi na kuendeleza michezo kama ilivyo kwa maeneo mengine", alisema.

Mgonza alisema maeneo mengi yanashiriki katika michezo lakini Kivule bado wako nyuma, ingawa kuna vipaji vingi ambavyo vinahitaji kuendelezwa.

Alisema kingine kilichotusukuma kufungua kituo hicho ni kwa sasa michezo inatoa fursa ya ajira kwa vijana, kwahiyo wanataka kuwasaidia vijana wengi wa Kivule na maeneo ya jirani kama vile Magole, Mbondole, Msongola, Majoe na Kitunda.

Mgonza alisema kituo hicho kinapokea mawazo na ushauri kutoka kwa wadau mbalimbali na wa michezo, ikiwemo mpira wa miguu, masumbwi, riadha, sarakasi, karate, kick boxing, na michezo mingine wawasilishe mawazo yao na yatapokelewa na kufaniwa kazi.

Pia alisema kituo hicho tayari kimepata usajili wa kuandaa mashindano ya michezo mbalimbali kwahiyo wanatarajia kuandaa tamasha la wazi kwaajili ya ufunguzi kituo hicho.

Mgonza amewaomba wananchi wa Kivule na wadau wote kutoka maeneo mbalimbali waje washiriki katika kuinua vipaji vya vijana kwani michezo ni ajira pia michezo ni afya.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...