Abdullatif Yunus Michuzi TV.
Serikali imetumia shilingi milioni 346.6 kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu ya Shule ya Sekondari Lyamahoro iliyopo kata Kaibanja Halmashauri ya Wilaya Bukoba Mkoani Kagera baada ya kuipandisha hadhi na kuwa na Kidato Cha Tano na Sita (High School)
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Shule hiyo Bi. Amina Haruna wakati akitoa ufafanuzi hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa miundombinu hiyo mbele ya Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini Dkt Jason Rweikiza wakati wa ziara yake ya kikazi shuleni hapo.
Mwalimu Haruna amesema kuwa mpaka sasa Bweni moja lenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 48 limekamilika hivyo wanategemea kupangiwa idadi hiyo ya wananfunzi wa kidato cha tano Mwaka huu, aidha Mkuu huyo wa Shule ameongeza kuwa yanajengwa mabweni mawili, madarasa manne, bwaro moja na vyoo.
Naye Mhe. Mbunge Dkt. Jason Rweikiza amemsihi Mkuu huyo kusimamia matumizi ya fedha zilizotolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya shule hiyo ili wanafunzi watakaochaguliwa kuanza masomo yao ya kidato cha tano katika shule hiyo wakute miundombinu imekamilika.
Mh Rweikiza amefika katika shule hiyo wakati wa ziara yake ya kuzitembelea shule za sekondari Jimboni humo ambapo ametembelea shule 10 na kuchangia shilingi mil 3 na laki saba(3,700,000)kwa ajili ya sukari ya wanafunzi na walimu na mipira miwili kila shule.
Aidha akizungumza na wanafunzi katika ziara hiyo amefafanua kuwa mwanafunzi huwezi kufaulu kama hausomi sana na huwezi kufeli kama unasoma sana hivyo kila mmoja ajikite katika kusoma sana.
Dkt. Jasson Rweikiza Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini akikagua Ujenzi wa Miundo mbinu ya Shule ya Sekondari ya Lyamahoro iliyopandishwa hadhi na kuwa High School wakati wa ziara yake Juni 06, 2021
Dkt. Jasson Rweikiza Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Lyamahoro Mara baada ya kuwasili Shuleni hapo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...