MKUU  wa Mkoa wa Arusha John Mongela ameitaka mahakama ya Afrika ya haki za binadamu ikafanye kazi zake kwa haki ili kuweza kupambana na matatizo yaliyopo katika bara  la Afrika.

Mongela ameyasema hayo alipokuwa  akimwakilisha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu, katika hafla ya kuchagua na kuwaapisha majaji wapya wa Mahakama hiyo.

Ameahidi ushirikiano ili kufanikisha malengo ya nchi wanachama na mahakama katika kuimarisha haki za binadamu.

Amesema amani na utulivu wa nchi yoyote popote Duniani inategemea sana mahakama kuwa za haki, kwani wanapambania matatizo ya Afrika ili bara liwe na amani na kujiletea maendeleo kwajili ya ustawi wa nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...