Mwenyekiti wa Vijana Taifa TLP, Eng.Aivan Maganza

HAIWEZEKANI Chama cha Siasa kuibuka na kusema kinataka masuala ambayo yapo kwenye Ilani ya chama Cha mapinduzi (CCM) bali wanachama waeleze changamoto katika jamii zinatatuliwa kwa njia gani?

Umoja wa Vijana Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) kupitia Mwenyekiti wa Vijana Taifa TLP, Eng.Aivan Maganza ameyasema wakati akizungumza na wandishi wa habari mkoani Dar Es Salaam leo. Amevitaka vyama vya upinzani nchini kuacha kumchonganisha Rais Samia Suluhu Hassan na wananchi kwa kitendo chao cha kudai katiba mpya ili hali suala hilo halipo katika ilani ya chama cha Mapinduzi (CCM).

Amesema kuwa kinachotakiwa ni kutatua changamoto katika jamii na si kuzungumzia vitu ambavyo havisaidii kutatua changamoto katika jamii.

"Tunachotaka ni Kwenye shida ya maji tunatoka vipi?, Kwenye mikopo ya Vijana tunatatuaje?, kuja kwenye jamii kueleza kuwa Umeme tutapelekaje vijijini, tunachotaka watoke waseme ni namna gani Reli ya Mwendo wa Haraka (SGR) inakamilikaje, watuambia mradi wa Rufiji unamalizikaje, hivi ndio vitu tunavyovitaka." Amesema Eng. Maganza

Hata hivyo alihoji Chama cha Siasa cha upinzani kinachodai Katiba Mpya, hilo fungu la fedha za kuanza kujadili Katiba Mpya linatoka wapi? Ingawa tumesikia bungeni wakati wa bunge la bajeti ya 2021/ 2021 hakuna bajeti ya kutengeneza Katiba mpya.

“Rais Samia alishasema kuwa atakutana na wapinzani, hizi haraka za wenzetu wa Chadema zinatoka wapi? huu ni wakati wa kumuacha Rais aliletee maendeleo Taifa letu ndipo hayo mambo mengine yafuate siku zote wanasiasa ndiyo wachochezi wa katiba mpya." Amesema Eng. Maganza

Amesema kuwa katika bajeti ya 2021/ 21 hakuna bajeti ya Katiba mpya hivyo kama chama cha siasa cha upinzani wasihangaika kuwasemea watanzania kuwa wanahitaji katiba mpya maana haina fungu la fedha.
Hata hivyo Eng. Maganza amesema kuwa kwa sasa vyama vya siasa viachane na dhana ya katiba mpya na waache Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania afanye kazi yake au wasubiri uchaguzi mwingine ndio waingine dhana ya katiba mpya.

Ameongeza kuwa wao kama TLP hawapo tayari kuona juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan za kuijenga nchi hii zikififishwa na wanasiasa wenzao aliodai kuwa wengi wao wanakuwa na ajenda tofauti na siyo zenye lengo la kujenga na kuleta umoja wa watu wote.

Licha ya hayo Eng. Maganza ameomba Vijana wakumbukwe kupitia mikoa yao hadi ngazi ya Halmashauri waweze kuwezeshwa kutokana na fursa zilizopo huko ili wachangie Taifa kupata Pato na wao pia, hivyo amewataka wakuu wa wilaya, Wakurugenzi kusimamia hilo ili taifa lipige hatua.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...