MKUU  wa mkoa wa Ruvuma  Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amefurahishwa na utendaji kazi wa Mkurugenzi wa halmashauri ya Mbinga Mji Grace Quintine kwa usimamizi mzuri wa fedha za  miradi ya maendeleo zinazotolewa na serikali na pia kwa kuweza kukusanya mapato ya ndani zaidi ya Tsh 2 .5 Bilioni kwa 115.42% na kufanikiwa kuvuka lengo la kukusanya Tsh 1.6 Bilioni

Pongezi hizo amezitoa leo wakati wa ziara yake ya kufatilia hoja mbalimbali za mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali katika halmashauri hiyo.

Akizungumza na madiwani wa halmashauri hiyo amesema mkurugenzi huyo ni mfano wa kuigwa kwenye halmashauri zote za mkoa wa Ruvuma kwa usimamizi wa fedha za miradi ya serikali na ukusanyaji mapato ya ndani ambapo amemtaka pamoja na kufanya vizuri asisite kuwachukulia hatua watumishi watakao fanya vibaya.

Aidha amempongeza mwenyekitiwa halmashauri hiyo , Kevin Mapunda,madiwani na watumishi kwa ushirikiano mkubwa wanaompa mkurugenzi huyo hivyo kuweza kuwa Halmashauri isiyo na migogoro na yenye kusimamia maendeleo ya Wananchi.

Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri hiyo Kevin Mapunda ameahidi kufatilia na kusimamia hoja zote zijibiwe kwa wakati na kuwaletea wananchi maendeleo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...