KAMPENI ya 'Twende Mjini na M-Pesa' inayoendeshwa na Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, imeendesha droo ya kwanza na kuwapata washindi watano waliojishindia bodaboda mpya (Boxer BM 125X) na mmoja akijishindia bajaji mpya aina ya a TVS King GS.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuchezeshwa kwa droo hiyo iliyodhuriwa na msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha na wanahabari leo Mkoani Dar es Salaam Afisa wa Masoko wa M-pesa Fredrick Mwamyalla amesema, kama walivyotoa ufafanuzi katika uzinduzi wa kampeni hiyo kwamba ndani ya wiki 8 watumiaji wa huduma ya M- PESA watapata fursa ya kujishindia bajaji, bodaboda na gari ya kisasa aina ya Toyota Corolla Cross (SUV) la mwaka 2021 ambalo litatolewa katika grand finale la kampeni hiyo.

Amesema kuwa kampeni ya Twende Mjini na M-Pesa ni ahadi ya Vodacom katika kuboresha maisha ya jamii na kampeni hiyo inawahusisha watumiaji wote wa M-pesa wakiwemo mawakala nchi nzima.

"Kampeni hii inawalenga watumiaji wote wa M-pesa ambao wataingia katika droo ya ushindani kwa kutumia huduma za M-Pesa kwa kutuma pesa kutoka akaunti ya benki kwenda M-Pesa, kutuma pesa kwa wateja wa Vodacom na wateja wa mitandao mingine, kulipa bili na huduma nyingine na moja kwa moja wataingia katika droo ya ushindi." Amesema.

Aidha amewataka wateja wa mtandao huo kupokea namba ya huduma kwa wateja 0754 100 100 ili kutopitwa na bahati zao na wataendeleza kampeni ya  kujitambulisha kwa wateja kupitia jumbe fupi 'Sms' pamoja na kupitia mitandao yao ya  jamii ili wateja na watumiaji wa huduma za M-Pesa wasipitwe na zawadi hizo.

Katika kampeni hiyo waliojishindia bodaboda ni Godfrey Mgeni (Morogoro,) Francis Kwale, Wakala wa huduma za M-Pesa (Dar es Salaam,)  Zanzibar gateway Wakala wa huduma za M-Pesa (Zanzibar,) Ramadhan Nkondo (Dar es Salaam) Pili Joseph (Dar es Salaam.) huku Bajaji mpya ikienda kwa Nyangije Basondole kutoka Dar es Salaam.Mchakato wa kuwapata washindi wa zawadi kupitia kampeni ya Twende Mjini na M-PESA ukiendelea katika ofisi kuu za Vodacom Tanzania Dar es Salaam.
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...