Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam 

KAMPUNI ya Michezo ya Kubashiri ya Sportpesa imezindua Promosheni maalum ijulikanayo kama’Mshiko Deilee’ kuelekea kwenye Michuano ya Ulaya (EURO 2020), Copa America na michezo ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (VPL) kwa kushirikiana na Mitandao ya Simu za Mkononi ya Tigo, Airtel na Vodacom.

Promosheni hiyo inahusisha kuwazawadia fedha kiasi cha Shilingi Elfu 10 kila mmoja kwa Watu 30, pia kutolewa Milioni 1 kwa kila wiki kwa washindi wa tatu, na baadae kutolewa Milioni 15,888,000/- kwa Wateja wa Sportpesa wanaotumia Mitandao hiyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Saalam, Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Sportpesa, Sabrina Msuya amesema Promosheni hiyo inaanza June 11, 2021 ikihusisha Michuano ya Euro, Copa America na Ligi Kuu Tanzania Bara, Sabrina amesema ili kuingia kwenye droo ya promosheni hiyo lazima ujisajili Sportpesa na kuweka pesa kwenye akaunti yako.

“Kila wiki watapatikana Washindi, tutakuwa na droo kwa wiki nne kwa awamu ndani ya mwezi mmoja, hii tunafanya ili kuleta hamasa kwa Watumiaji wa Mitandao ya Simu, Wateja wa Sportpesa waendelee kucheza droo zetu”, amesema Sabrina 

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mtandao wa Vodacom, ambaye ni Meneja Mauzo wa M-Pesa, Kelvin Nyanda amesema amewaasa Wateja wao kucheza Promosheni hiyo ili kuingia kwenye droo ya kila siku, kila wiki na mwezi ili kujishindia, Nyanda amewaasa Wateja kucheza Promosheni hiyo kwa kuafuata maelekezo

Naye Mwakilishi kutoka Mtandao wa Tigo, Fabian Felician amesema wameshirikiana na Sportpesa ili kuwa nafasi wateja wao kujishindia pesa hizo zinazotolewa kwenye Promosheni hiyo.

Promosheni hiyo imeletwa na Sportpesa ili kuwapa nafasi Wateja wa Mitandao ya Simu kuwapa tabasamu Wananchi na kuwaondolea matatizo madogo madogo katika maisha ya kila siku.

Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Sportpesa, Sabrina Msuya akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa Promosheni maalum ijulikanayo kama’Mshiko Deilee’ kuelekea kwenye Michuano ya Ulaya (EURO 2020), Copa America na michezo ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (VPL) kwa kushirikiana na Mitandao ya Simu za Mkononi ya Tigo, Airtel na Vodacom

Picha ya PamojaMichuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...