Benki ya Stanbic Tanzania imetoa msaada wa vifaa na fedha wenye thamani ya Sh9.2 millioni kwa klabu ya Waandishi wa Habari za Michezo nchini, Taswa SC).

Taswa SC inatarajia kucheza mchezo  wa kirafiki dhidi ya timu ya Bunge FC ambapo Mkuu wa Masoko wa benki ya Stanbic Tanzania, Desideria Mwegelo amesema msaada huo utafanikisha vyema ziara hiyo ya mkoa wa Dodoma.

Mwegelo amesema kuwa benki yao  inatambua mchango wa Taswa SC katika maendeleo ya michezo nchini pamoja na masuala ya afya.

“Michezo ni moja ya njia ya kujenga afya ya mwili katika jamii. Benki yetu mbali ya kusaidia michezo, pia inasaidia masuala ya afya, tunaamini kwa msaada huu, timu itafanya vizuri katika mchezo huo,” alisema Mwegelo.

Alisema kuwa benki yao inajisia fahari zaidi kushirikiana na Taswa SC kwani  wanafanya hivi kwa mara ya pili.

“Msaada huu pia ni sehemu ya benki ya Stanbic Tanzania kujishughulisha na masuala ya shughuli za kijamii. Tunawaomba wachezaji wa Taswa SC watuwakilishe vizuri siku ya mchezo huo,” alisisitiza Mwegelo.

Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary aliipongeza benki ya Stanbic Tanzania kwa msaada huo ambao utwafanya kufanya safari yao kwa uhakika zaidi mbali ya kucheza mechi.

Majuto alisema kuwa klabu ilikuwa njia panda kusafiri kwenda Dodoma na  maada huo umewahamasisha wachezaji kufanya vyema.

 “Msaada umekuja wakati muafaka ambapo klabu ilikuwa inahitaji kusafiri na kucheza mechi dhidi ya timu ya Wabunge. Naishukuru sana kwani ndoto yetu ya miaka mingi kucheza na Bunge FC mkoani Dodoma itatimia,” alisema Majuto.

 Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano  cha benki ya Stanbic Tanzania, Desideria Mwegelo (Kulia)akikabidhi mfano wa hundi wenye thamani  ya Sh9.2 millioni  kwa mwenyekiti wa klabu ya Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa SC) Majuto Omary. Fedha hizi ni kwa ajili ya kugharimia vifaa na ziara ya Dodoma kucheza mechi dhidi ya timu ya Bunge FC.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...