Mkurugenzi wa Umoja wa Wahitimu Wajasiliamali Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine SUGECO Revocutus Kimario akitoa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana zaidi ya 400 kutoka vyuo vya kati vya kilimo na baadhi ya vikundi vya wakulima mkoani Mbeya.
Mkufunzi wa chuo cha kilimo Uyole( MAT-UYOLE)mkoani Mbeya Betina Mwakasanga akiangalia bidhaa zinazozalishwa na wanachuo wa chuo hicho.
Mkuu wa chuo cha kilimo Uyole mkoani Mbeya wa tatu kulia (Suti Nyeusi) Akiangalia bidhaa inayozalishwa na mjasiliamali kutoka Mbeya katika maonyesho yaliyowahusisha wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya kilimo mkoani Mbeya yenye lengo la kuwaunganisha wakulima na masoko lakini pia kutambulisha uwepo wa ofisi za SUGECO maeneo ya Chuo cha kilimo Uyole .
Baadhi ya wananchuo wakipewa maelekezo ya teknolojia mbalimbali na bidhaa zinazozalishwa na umoja wa wahitimu wajasiliamali chuo kikuu cha kilimo Sokoine SUGECO .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...