Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
Chama
cha wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo (TCCIA ) ,Mkoani Pwani
,kimewahimiza wafanyabiashara na wakulima kujiunga uanachama ili
kujiimarisha na kuongeza nguvu ya pamoja kujiinua kiuchumi.
Pia
kimewaasa vijana kuchangamkia fursa hiyo ili waweze kujifunza na kupata
uelewa wa kujiajiri kibiashara kupitia wabobezi wa viwanda na
wafanyabiashara walio kwenye chama hicho.
Akizungumzia
hatua wanazozichukua kukiinua chama na vipaombele ,makamu mwenyekiti
-Biashara -Fadhil Gonzi alieleza ,mkoa umesheheni viwanda ni wakati wa
wenye viwanda hao kuwa sehemu ya chemba yao ili kujikwamua kimaendeleo .
Suala
jingine alieleza ,ni wanachama kupata fursa ya elimu ya biashara na
kuwa na elimu ya nidhamu ya fedha ili kulinda biashara zao.
Gonzi
,alieleza kwamba pia watajitahidi wanachama wao kufikia soko la ndani
na nje kwani ukosefu wa soko imekuwa ni changamoto na kilio cha kila
kukicha.
"Kwanini Pwani
tushindwe kuandaa maonyesho makubwa kama sabasaba ,mkoa ulishaanza na
ulifanikiwa kwa kiasi chake lakini bdo tuna kazi ya kuwa kuandaa
maonyesho makubwa zaidi ili kujitangaza na kubadilishana uzoefu"
alifafanua Gonzi .
Mwenyekiti
wa TCCIA Pwani ,Saidi Mfinanga alifafanua akiwa kama mtaalamu wa
masuala ya fedha ,uchumi na ushauri wa kodi atahakikisha wanashirikiana
na wadau mbalimbali kutatua changamoto ya ukosefu wa masoko na kuwapa
elimu ya biashara wanachama .
Alisema
ni imani yake kujenga ushirikiano baina ya sekta binafsi na Serikali
kwa kuhamasisha wafanyabiashara kujiunga kwenye Sacco's na chama.
Mfinanga
alielezea ,ajira bado ni changamoto duniani na Tanzania, hivyo ni
muhimu kuwajengea uwezo vijana kuboresha uelewa wao katika biashara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...