Na John Mapepele, Mtwara

Serikali imesema wanafunzi sita watakaofanya vizuri mashindano ya UMITASHUMTA upande wa Riadha yanayoendelea kwenye viwanja vya Chuo cha Ualimu mjini Mtwara watapelekwa katika mashindano ya kimataifa ya Shirikisho la Michezo ya Wanafunzi Duniani (ISSF) yatakayoanza Septemba mwaka huu nchini Slovenia

Hayo yasemwa na Mratibu wa UMITASHUMTA na UMISSETA Taifa, Leonard Thadeo wakati akiongea na waratibu wa michezo, makocha na walimu wa michezo kutoka mikoa yote inayoshiriki mashindano hayo ambapo amesisitiza kuzingatia kanuni zote za michezo huu ili kuwapata wachezaji wenye nidhamu na sifa watakaopeperusha vema bendera ya nchi yetu

“Hii ndiyo dhana ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa ya kutaka ufundishaji michezo kuanza kwenye shule za Awali,Msingi, Sekondari na Vyuo ili kupata washiriki wengi walionolewa vizuri kwenye mashindano ya kimataifa kama yanavyofanya mataifa makubwa”. Amefafanua Thadeo

Mhe. Majaliwa alisema wakati akifungua mashindano haya kuwa kupitia michezo na sanaa, wanafunzi watafunguliwa vipaji vyao ambavyo vikiendelezwa vema vitawapatia manufaa mazuri ya kitaaluma na ajira.

Katibu Mkuu wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt,Hassan Abbasi amesisitiza kuwa Serikali imejipanga kuanzisha na kuboresha vyuo vya michezo nchini ili kupika na kunoa vipaji vya wanamichezo na hatimaye kuviuza duniani

“Mikakati ya Serikali kwenye Sekta ya Michezo kwa sasa ni kuhahakisha taaluma ya michezo inaboreshwa na inatolewa kwa kiwango cha kimataifa ili wanamichezo wetu wawe kwenye viwango vya kimataifa, tukumbuke kuwa michezo ni sayansi. “Amefafanua Dk Abbasi

Michezo ya leo kwenye riadha imehusisha mita 100 kwa wavuala na wasichana, mita 100 kwa wenye ulemavu ambayo imefika fainali na kumalizika, mita 1500 kwa wavulana na wasichana relay mita 400x4 na mchezo wa kurusha tufe ambao umefikia fainali ambapo mkoa wa Kigoma kwa upande wa wavulana na Manyara kwa wanawake walishinda. 



Wanariadha kutoka mikoa mbalimbali wakiwa kwenye mashindano ya mbio za mita 1500 katika viwanja vya Chuo cha Walimu leo Juni 14, 2021 mjini Mtwara.


  Mratibu wa mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA Leonard Thadeo akitoa maelekezo kwa waamuzi na waratibu wa michezo wa mikoa mbalimbali iliyoshiriki mashindano hayo leo Juni 14,2021 mjini Mtwara



 Makatibu wakuu wa Wizara (Habari, TAMISEMI, na Elimu) zilizoratibu mashindano ya UMISHUMTA na UMISSETA na Wakurugenzi wakikagua miundombiunu ya mashindano hayo kabla ya kuanza rasmi Juni 7,2021 mjini Mtwara

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...