Mkuu wa kitengo cha ukaguzi wa vipodozi kutoka Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDA) Salim Hamad Kasim (wakatikati) akiwa na waandishi wa habari wakitizama tarehe ya mwisho wa matumizi ya tambi aina ya pasta walizozikamata nyumbani kwa mfanya biashara Ramadhani Khatibu Juma Shakani Nnje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Wafanyakazi wa Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar wakifungua mlango wa Godauni la mfanya biashara Ramadhani Khatib liliopo kwa Mombasa kwa Mchina ili kukagua bidaa zilizokuwemo.

**************************

Na Ali Issa Maelezo 18/6/2021

Zaidi ya bidhaa zenye thamani ya shilingi milioni 200 zimekamatwa na Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDA) kwa kukosa kiwango cha uingizwaji nchini pamoja na kupitiwa na muda.

Akitoa taarifa kwa wandishi wa habari mara baada ya ukaguzi wa bidhaa hizo Mkaguzi Mkuu kutoka Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi Suleiman Akida Ramadhani amesema bidhaa hizo zimekamatwa katika maeneo ya Shakani na Kwamchina.

Alisema bidhaa hizo zimeingizwa kutokea nchini Ukrain zimeingia Zanzibar bila ya kufanyiwa ukaguzi na Wakala husika jambo ambalo ni kinyume na utaratibu uliowekwa.

Alifahamisha kwamba bidhaa hizo hazikuwa na vifungashio vyenye lugha inayofahamika na kutoa maelekezo pia zimeshapitwa na muda na ni hatari kwa matumizi ya binadamu.

Akizitaja bidhaa hizo nipamoja na Tambi aina ya Pasta, makoronya, sabuni mbalimbali na biskuti ambazo zimeingia nchini mwaka 2019 na hazikuwahi kukaguliwa kupitia Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi.

Mkuu huyo aliwataka wafanyabishara kufuata sheria na taratibu za uingizaji wa bidhaa nchini ili kuepuka hasara pamoja na kulinda afya ya mtumiaji.

“Mfanya biashara yoyote ni lazima akubali maagizo anayopewa na taasisi husika kabla ya kuingiza bidhaa nchini na sio kumuachia wakala kutoa mizigo kinyemela kwani hupelekea hasara pale zitakapoangamizwa” alisema Mkaguzi huyo

Nae Mfanyabiashra wa bidhaa hizo Ramadhani Khatibu Juma amesema amekubali kupokea uamuzi utakaotolewa na taasisi hiyo ili kuepuka madhara ambayo yanaweza kumpata mtumiaji.

Aidha alisema kuwa suala la kutokaguliwa bidhaa hizo linatokana na kumuachia wakala wake ambaye alimthibitishia kuwa amelipia sehemu zote zinazo stahiki kulipiwa na kufanyiwa vipimo kwa matumizi ya binaadamu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...