Wanafunzi wa kozi ya Astashahada ya uzamili kutoka Chuo cha Diplomasia (CFR) na wakufunzi wao wamefanya ziara ya mafunzo kwa kutembelea Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dodoma na kuzungumza na watendaji wa Wizara kwa ajili ya kujifunza namna Wizara watendaji wa Wizara wanavyotekeleza diplomasia ya uchumi kupitia kazi zao.
Wanafunzi hao kutoka kampasi ya Dar es Salaam na Dodoma walipata nafasi ya kusikiliza mada za muundo na majukumu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001.
Akizungumza wakati wa kuwakaribisha wanachuo hao kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mkurugenzi wa Kitengo cha wa Diaspora Balozi Anisa Mbega aliwataka wanachuo hao kusikiliza kwa umakini mada zitakazotolewa na watendaji wa Wizara ambao wanafanya shughuli za kidiplomasia kwa vitendo ili kujiongezea ujuzi zaidi.
Balozi Anisa aliwaambia wanachuo hao kuwa Wizara inaona fahari kuwa na chuo hicho kwani kinawezesha upatikanaji wa elimu ya diplomasia kwa wananchi wengi na kuwataka wanachuo hao kuitumia elimu wanayoipata kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla
Akizungumza kukamilisha mazungumzo kati ya wanachuo hao na watendaji wa Wizara Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama Balozi Stephen Mbundi aliwataka wanachuo hao kuwa tayari na kujiandaa na dunia ya sasa ili waende na wakati uliopo na aliwaahidi kuwa Wizara iko tayari muda wowote kuwasaidia ili waweze kuitendea haki elimu waliyoipata.
Wanachuo hao na wakufunzi wao walikuwa na ziara ya siku mbili jijini Dodoma ambapo siku ya kwanza walienda kutembelea Bunge kwa mwaliko wa Naibu Waziri –Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Nassor Mbarouk na kujionea jisni Bunge la Tanzania linavyoendesha shughuli zake.
Mwakilishi
wa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Mkurugenzi wa Kitengo cha wa Diaspora Balozi Anisa Mbega
akizungumza kuwakaribisha Wanafunzi wa kozi ya Astashahada ya uzamili
kutoka Chuo cha Diplomasia (CFR) na wakufunzi wao waliotembelea Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa ajili ya
kujifunza
Mkurugenzi
wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi akizungumza baada
ya kukamilika kwa mazungumzo kati ya Wanafunzi wa kozi ya Astashahada
ya uzamili kutoka Chuo cha Diplomasia (CFR) na wakufunzi wao
waliotembelea Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
kwa ajili ya kujifunza
Baadhi
ya Wanafunzi wa kozi ya Astashahada ya uzamili kutoka Chuo cha
Diplomasia (CFR) waliotembelea Wizarani kwa ajili ya kujifunza shughuli
mbalimbali za Wizara wakisikiliza mawasilisho mbalimbali yaliyokuwa
yakitolewa na watendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki

Wakufunzi
wa Chuo cha Diplomasia (CFR) wakisikiliza mawasilisho mbalimbali
yaliyokuwa yakitolewa na watendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, walipowaongoza Wanafunzi wa kozi ya
stashahada ya uzamili kutembelea Wizarani kwa ajili ya kujifunza
shughuli mbalimbali za Wizara
Baadhi
ya Wanafunzi wa kozi ya Astashahada ya uzamili kutoka Chuo cha
Diplomasia (CFR) walotembelea Wizarani kwa ajili ya kujifunza wakiwa
katika picha ya pamoja na watendaji wa Wizara ya Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dodoma

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...