Serikali imewataka wananchi na vyombo mbalimbali kushiriki pamoja katika kulinda miundombinu dhidi ya watu waovu na wasio wazalendo wanaoiharibu kwa lengo la kuuza chuma chakavu.

 Wito huo umetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Hamad Hassan Chande leo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu mesema hayo leo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Mhe. Fakharia Shomar Khamis aliyetaka kufahamu Serikali imejipangaje kukabiliana na wizi wa vyuma unaosababishwa na kushamiri kwa biashara ya chuma chakavu nchini

 Chande alisema kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004, kupitia Vifungu vya 133 -139, Serikali imeweka kanuni za udhibiti wa taka hatarishi ikihusisha ukusanyaji, usafirishaji na uhifadhi wa taka hatarishi.

 Alisema pamoja na biashara ya vyuma chakavu kusaidia kuziondosha taka hizi katika mazingira na kutengeneza mazingira safi na salama kwa afya ya binadamu lakini Serikali imekuwa ikitoa miongozo mbalimbali pamoja na elimu kwa jamii katika ulinzi wa miundombinu.

 Hata hivyo Naibu Waziri Chande alibainisha kuwa vyuma chakavu ni malighafi ya viwanda hasa vile vya nondo na hivyo kuweza kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

 Serikali kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi imekuwa ikifanya ukaguzi wa mara kwa mara katika viwanda ili kudhibiti suala la uhujumu wa miundombinu hiyo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Muungano na Mazingira), Mhe. Selemani Jafo akiwa na Naibu wake, Mhe. Hamad Hassan Chande wakati wa kipindi cha maswali na majibu bungeni jijini Dodoma leo Juni 9, 2021.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Muungano na Mazingira), Mhe. Selemani Jafo akifafanua jamnbo wakato wa kipindi cha maswali na majibu bungeni jijini Dodoma leo Juni 9, 2021.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Muungano na Mazingira), Mhe. Selemani Jafo akimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Khamis Hamza Chilo wakati wa kipindi cha maswali na majibu bungeni jijini Dodoma leo Juni 9, 2021.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Hamad Hassan Chande akijibu maswali leo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu mesema hayo leo bungeni jijini Dodoma leo Juni 9, 2021.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...