MAHAKAMA ya Hakimu mkazi Pwani (Kibaha)  imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela Ridhiki Omary Marimbwa kwa  kosa la kusafirisha kilo 21.86 za  dawa za kulevya aina ya bangi.

Hukumu hiyo ilitolewa  tarehe 29 mwezi Julai 2021 na  hakimu Mhe. Joyce Mushi baada ya mtuhumiwa  kutiwa hatiani kwa kosa la kusafirisha Dawa za kulevya aina ya bangi

Akisoma hukumu hiyo mheshimiwa Joyce Mushi amesema kwamba, upande wa Jamhuri umethibitisha kosa hilo pasi na kuacha shaka hivyo imemtia mshtakiwa hatiani. Kwa kuwa, makosa ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya yamekithiri mkoani Pwani,  hana budi kumpa mshtakiwa adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine.

Wakati akijitetea mshtakiwa aliiomba mahakama kumpunguzia  adhabu  kwani ana familia yenye watoto wadogo wanaomtegemea.

Pamoja na hukumu hiyo Mhe. Mushi aliamuru kutaifishwa kwa pikipiki iliyotumika kutekeleza uhalifu huo pamoja na kuteketezwa kwa bangi iliyokamatwa.

Mshtakiwa alikamatwa tarehe 18 mwezi Agosti  mwaka 2020  kwenye hifadhi ya wanyamapori ya Selous mkoani Pwani akisafirisha dawa hizo.

Mshtakiwa ametiwa hatiani kwa Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Na. 5 ya mwaka 2015 kama ilivyorejewa mwaka 2019.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...