WAZIRI wa Maji Mhe.Jumaa Aweso,akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha watendaji  wa wizara ya maji na taasisi zake katika kada ya manunuzi na ugavi, uhasibu na wakaguzi wa ndani kilichofanyika leo Julai 8,2021 jijini

Aweso amesisitiza watumishi hao kuachana kabisa na michakato isio na ulazima inayochelewesha miradi ya Maji na kuwataka kujipanga vilivyo katika kufanikisha utekelezaji wa miradi kwa haraka na viwango.

Aweso amewataka watumishi hao kwenda kufanya kazi kwa mujibu wa sheria,kanuni na taratibu zilizowekwa huku akiwasisitiza zaidi kutenda haki,kuzingatia nidhamu na kuboresha mahusiano mazuri katika utekelezaji wa majukumu yao.

‘’Pasipo na nidhamu mipango mizuri haiwezi kufanikiwa nidhamu ianze kwa mtu mmoja mmoja, dhamira yetu kwenye wizara ya maji ni kuhakikisha miradi ya maji itekelezwe kwa ubora na kumalizika kwa wakati”amesema Aweso

Aidha, Aweso amesema kuwa ukiacha Bajeti ya sh Bilion 680 waliopewa na Serikali,Rais Samia  amewaongezea sh billion 207 ili kuboresha sekta ya Maji kwa sababu ameipa kipaumbele.

‘’Tusishangilie tu kuwa tumeongezewa fedha halafu mkajenge mianya ya kutumia fedha vibaya,hizi fedha haziliki ,ukiamua kula kwa makusudi hizi fedha za mama Samia jela inakuita’’amesisitiza Aweso

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...