Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

BAADA ya kufunguliwa Dirisha la Usijali na Uhamsiho wa Kimataifa kwa Klabu za Tanzania kuanzia Julai 19, 2021 hadi Agosti 31, 2021, Matajiri wa Chamazi, Klabu ya Azam FC imetangaza kuachana na Wachezaji wake wanne wa kigeni, Obrey Chirwa, Mpiana Monzinzi, Ally Niyonzima na Yakubu Mohammed ambao wamefika makubaliano pande zote mbili kutoendelea kuitumikia Klabu hiyo.

Kupitia Mitandao yao ya Kijamii, Azam FC wametoa taarifa ya kuwashukuru Wachezaji hao ambao ilikuwa nao Kikosi kwa misimu kadhaa ya Mashindano.

“ThanksAll Tumefika makubaliano ya pande mbili ya kuachana na wachezaji wetu wanne wa Kimataifa. Wachezaji hao ni beki wa kati, Yakubu Mohammed, Kiungo Ally Niyonzima, Mshambuliaji, Mpiana Monzinzi na Obrey Chirwa, ambaye mkataba wake umemalizika”.

“Azam FC tunawashukuru kwa mchango wao waliotoa katika klabu hii bora kipindi chote walichokuwa nasi na tunawatakia kila la kheri huko waendako”.

Kuelekea msimu ujao wa Mashindano, Azam FC hadi sasa imetangaza usajili wa Wachezaji wanne wa Kimataifa kuboresha Kikosi chao kilichomalizq nafasi ya tatu msimu uliopita. Wachezaji waliosajiliwa kwa ajili ya msimu ujao Kikosini hapo ni Kiungo Mkabaji wa Kimataifa wa Zambia, Paul Katema akitokea Klabu ya Red Arrows ya nchini humo, Kiungo Mshambuliaji wa Kimataifa wa Kenya, Kenneth Muguna kutoka Gor Mahia nchini humo.

Wengine ni Mshambuliaji wa Kimataifa wa Zambia, Rodgers Kola kutoka Klabu ya Zanaco  ya nchini humo, pia imemsajili Beki wa pembeni wa Kimataifa wa Tanzania, Edward Charles Manyama kutoka Klabu ya Ruvu Shooting FC ya hapa hapa nchini.

Azam FC msimu ujao itacheza Mashindano ya Kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) baada ya kushika nafasi ya tatu katika Msimamo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (VPL), huku Tanzania ikiingiza timu nne katika Michuano ya Kimataifa.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...