Na Mwandishi wetu, Dar

Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) limemuapisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula kuwa Mjumbe wa Baraza la Maamuzi wa Bunge hilo leo tarehe 6 Juni 2021 katika mkutano uliofanyika kwa njia ya Mtandao jijini Dar es Salaam

Akizungumza mara baada ya kuapishwa na Spika wa Bunge hilo Mhe. Martin Ngoga leo tarehe 6 Juni 2021 katika mkutano uliofanyika kwa njia ya Mtandao jijini Dar es Salaam Balozi Mulamula amesisitiza umuhimu wa bunge hilo kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano kutokana na umuhimu  na matarajio ya Wananchi kwa Bunge hilo.

Aidha Balozi Mulamula amepongeza jitihada zinazofanywa na Bunge hilo kuendelea na vikao vyake kwa njia ya mseto ikiwa ni pamoja na kukutana ana kwa ana ama kwa njia ya mtandao licha ya changamoto ya uwepo wa ugonjwa wa UVIKO – 19 hali inayoonesha dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi.

“Wananchi wamekuwa na matarajio makubwa sana kupitia Bunge hili la Afrika Mashariki kiuweza kuona faida na mambo mazuri yanayofanyika kupitia jumuiya hii ya Afrika Mashariki,” Amesema Balozi Mulamula.





Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula ameapa kuwa Mbuge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) na mjumbe wa Baraza la Maamuzi. Balozi Mulamula ameapa kuwa mbuge wa EALA leo tarehe 6 Juni 2021 katika mkutano uliofanyika kwa njia ya Mtandao jijini Dar es Salaam. Picha na Mambo ya Nje.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...