*Waziri Mwigulu azishauri benki kupunguza riba
* Afafanua suala la ufilisi wa dhamana kwa wateja

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

WAZIRI wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba amezindua rasmi benki ya Biashara Tanzania (TCB,) ambayo ni muunganisho kwa benki ya TIB na TPB huku lengo kuu likielezwa ni kuundwa kwa benki kuu ya Serikali na ushindani ambayo itatoa huduma zote za kibenki na biashara kama benki nyingine za kibiashara duniani.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Waziri Nchemba amesema benki hizo zimeunganishwa kwa kuzingatia ushauri na matakwa ya kisheria hivyo wafanyakazi wa benki hiyo mpya hawana budi kulitendea haki kwa jina  hilo kwa kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii, ushindani na ubunifu wa hali ya juu kwa misingi ya benki hiyo ya taifa ya biashara nchini.

Amesema, benki hiyo itahudumia wateja wateja wote na wafanyabashara waliokuwa TPB na TIB na itatoa huduma kwa vwang vya kuhakksha mageuzi zaidi yanaendelea katika sekta ya fedha nchini ili kujenga uchumi imara na shindani katika viwango vya kimataifa.

" Hizi ni jitihada za Serikali katika kujenga uchumi wa taifa kwa kuzingatia uadlifu na ubunifu na sisi Wizara ya fedha, benki kuu tutatoa ushirikiano katika kuijenga benki ya biashara nchini TCB.'' Amesema Mwigulu.

Aidha Wazri Nchemba amezishauri benki zote nchini kushusha riba katika hatua zilizopo mikononi mwao na hiyo ni pamoja na kuangalia namna wanavyofilisi mali za wateja pindi wanaposhindwa 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...