NA TIGANYA VINCENT

MKUU wa Wilaya ya Tabora Dkt.Yahya Nawanda amesema hatasita kuwachukulia hatua za kisheria kwa watu ambao hawana sifa ya kupokea fedha kwa ajili walengwa wa mpango wa kunusuru kaya Maskini (TASAF)

Aliota kauli hiyo jana wakati wa Kikao kazi cha kujenga uelewa kuhusu kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya TASAF na kutoa mwongozo wa utambuzi na uandikishaji wa kaya za walengwa katika eneo la Utekelezaji kwenye Manispaa ya Tabora.

Alisema fedha hizo zinatolewa na Serikali kwa ajili ya kuziwezesha kaya maskini ziweze kujikimu katika mahitaji muhimu ikiwemo upatikanaji wa huduma za chakula, elimu , afya ili ziliweze kushiriki vizuri katika shughuli nyingine za maendeleo.

Dkt. Nawanda aliwataka TASAF kushirikiana na Madiwani wa Manispaa ya Tabora wakati wa utambuzi na uandikishaji wa Kaya Maskini ili kuepuka kuwaacha walengwa.

Alisema kitendo cha kuwaacha walengwa kinaweza kusababisha lawama na malalamiko kwa Madiwani ambao ni Wawakilishi wa wananchi na wako karibu na wanatambua hali halisi za watu wao.

“Tumieni mbinu shirikishi kuwabaini walengwa ili malalamiko yalipo kwa baadhi ya kaya maskini yasiweze kujirudia tena” alisisitiza.

Kwa upande wa Afisa Mfuatiliaji Manispaa ya Tabora Nisalile Mwaipasi alisema kwamba madiwani wanawajibu mkubwa kuhakikisha wanashirikina ili kuweze kutimiza lengo la serikali ya kutambua kaya masikini .

‘’sisi wote tunajenga nyumba moja hakuna haja ya kugombea fito jambo ambalo litarudisha nyumba malengo ya serikali ‘’alisema Mwaipasi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...