MKAZI wa Mburahati, Jijini Dar es Salaam, Jamali Nang'utikile(45) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na shtaka moja la kusafirisha dawa za kulevya aina Heroin zenye uzito wa gramu 494.52.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa Serikali, Ashura Mzava mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ritha Tarimo inadaiwa, Juni 2021, huko Mburahati, wilaya ya Ilala mshtakiwa alikutwa akisafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin zenye e uzito wa gramu, 494.52 huku akijua kufanya hivyo ni kosa na kinyume cha sheria.

Hata hivyo mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za dawa za kulevya.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi.

Agosti 4, 2021 itakapotajwa tena.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...