Na Amiri Kilagalila,Njombe

Edita Mangita (40) mkazi wa mtaa wa Matema kata ya Maguvani mjini Makambako amefariki dunia baada ya kujifungia na jiko la mkaa Katika kibanda chake cha biasahara.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamisi Issa amesema tukio hilo limetokea Julai 28,2021 ambapo marehemu Editha aliamua kubaki na kulala katika kibada chake cha biashara Ili kuwahi wateja wake wa asubuhi.

Aidha kamanda Issa amewataka wananchi wa mkoa wa Njombe kuacha kulala na majiko ya mkaa ndani huku akitoa wito kwa wataalamu wa afya kuendelea kutoa elimu kuhusu madhara hayo Ili jamii.

Hivi karibuni mjini Njombe kulitokea kifo cha watu wawili wapenzi baada ya kulala na jiko la mkaa ili kupunguza baridi katika chumba chao.

Kamanda Issa ametaja tukio lingine la mwanamke mmoja Imelda Mgeni ametelekeza mtoto mwenye umri wa miezi mitatu kwa mume wake naye kwenda kusikojulikana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...