Mnadhimu Mkuu wa  Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Luteni Jenerali Yakoub Mohamed

Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania JWTZ   kwa kushirikiana na Jeshi la Marekani wanatarajia kufanya Mafunzo Maalum kukabiliana na Vitendo vya Uhalifu ikiwemo Ugaidi.

Hafla ya Kufungua Mafunzo hayo umefanyika leo Julai 28 katika kituo cha Ulinzi wa Amani  na Mkuu wa Kamandi ya Afrika wa Jeshi la Marekani  Jenerali  Stephen Townsend Kunduchi Dar es Salaam.

Jenerali Toensend amesema Tanzania na Marekani zimekua na ushirikiano katika mambo mbalimbali hivyo ni sehemu sahihi katika Mafunzo hayo maalumu.

Kwa Upande wake  Mnadhimu Mkuu wa  Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Luteni Jenerali Yakoub Mohamed amesema jeshi la Marekani limekua likishirikiana vyema na Jeshi la Wananchi wa Tanzania katika Mafunzo mbalimbali

Mafunzo Hayo maalumu ya Mwezi mmoja kwa ajili ya Kukomesha Vitendo vya Uhalifu  ikiwemo,  Ugaidi na vitendo vingine kama hivyo ambavyo vimekua vikitokea katika Mataifa Mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...