Na Zainab Nyamka, Michuzi TV

KESI ndogo namba 305 ya kusimamisha mchakato wa uhaguzi Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) kutolewa maamuzi Julai 16.

Chini ya Jaji Edwin Kakolaki wa Mahakama Kuu Jijini Dar es Saalaam, amesema kesi hiyo ataitolea maamuzi kamili yatatolewa Julai 16 saa 8:00 mchana.

Jaji Edwin Kakolaki amesema amesikiliza pande zote mbili baada ya kuwasilishwa kwa hoja zao.

Awali kesi hiyo ilisikilizwa kwa mara ya kwanza Julai 3 na leo imesikilizwa kwa mara ya pili kuanzia saa 3:18 asubuhi hadi saa 7:00 mchana alipoeleza kuitolea uamuzi Julai 16.

Wakili upande wa Ally Salehe ambaye ni moja ya wagombea walioeunguliwa, Frank Chacha amesema kesi ina mwenendo mzuri na kila upande umepeleka hoja zao na wanachosubiri ni uamuzi wa Mahakama katika kesi ndogo namba 305 kama mchakato wa uchaguzi huo uendelee au usitishwe.

Ally Salehe alifungua kesi Mahakama Kuu kupinga mchakato huo sanjari na katiba ya TFF. Uchaguzi mkuu wa TFF unatarajiwa kufanyika Agosti 7 mjini Tanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...