Naibu
Waziri wa Nishati Mhe. Wakili Stephen Byabato ameielekeza TANESCO
ifikapo tarehe 15 Agost, 2021 umeme uwe umefika kwenye kituo cha Afya
cha Nyaruyoba kilichopo wilayani Kibondo mkoani Kigoma.
Naibu
Waziri Byabato ameyasema hayo kufuatia maelekezo ya Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpango alipokuwa
katika ziara ya kikazi mkoani Kigoma tarehe 17 Julai, 2021 mara baada ya
kuzindua Kituo cha Afya cha Nyaruyoba.
Awali,
Mkurugenzi wa Halmshauri ya Kibondo alimueleza Makamu wa Rais kuhusu
changamoto wanazokutana nazo kuhusiana na kukosekana kwa umeme katika
kituo cha Afya cha Nyaruyoba na kuomba kupatiwa umeme katika kituo
hicho.
Naibu Waziri
Byabato, amewaambia wananchi wa Nyaruyoba kuwa, gharama za kuunganishiwa
umeme ni shilingi 27,000 tu na kuwa hakuna kuuziwa nguzo wala
transforma.
Aidha, Naibu
Waziri Byabato ameiagiza TANESCO ifungue ofisi ya malipo Nyaruyoba ili
kuwapunguzia wananchi kwenda umbali mrefu kulipia gharama za
kuunganishiwa umeme.
Pia,
Naibu Waziri Byabato amesema ifikapo Oktoba 2022, Grid ya Taifa itakuwa
imefika Kigoma na kuimarisha hali ya upatikanaji wa umeme.
Ameongeza
kuwa, vijiji vyote ambavyo havijaunganishiwa umeme wilayani Kibondo na
Kigoma kwa ujumla vitakuwa vimepatiwa umeme ifikapo mwezi Desemba 2022.
Naibu
Waziri Byabato, amewataka TANESCO waendelee kuwaunganishia umeme wateja
ambao bado hawajaunganishiwa umeme wakati wa Mradi.
Vile
vile akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo la Halmashauri ya
mji wa Kasulu uliofanywa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango tarehe 17 Julai, 2021, Naibu
Waziri Byabato ameielekeza TANESCO kuongeza jitihada za kufunga mashine
moja ya MW 1.25 ili kuboresha zaidi upatikanaji wa umeme wilayani
Kasulu.
Malekezo ya
Naibu Waziri ni kutokana na maelezo ya Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini
aliyomweleza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Dkt.Philip Isdor Mpango kuhusu changamoto za upatikanaji wa umeme katika
wilaya ya Kasulu.
Naibu
Waziri Byabato ameshiriki katika ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kuanzia tarehe 15 Julai hadi 18 Julai, 2021 Mkoani
kigoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...