Na Abel Paul-Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishina msaidizi wa Polisi ACP JUSTINE MASEJO akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake leo amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linaendelea kuwashukuru wananchi wote wa Mkoa wa Arusha kwa ushirikiano wanao endeleea kuutoa na kuonyeshea kwa Jeshi la lao la Polisi.

ACP-Masejo amesema kuwa hali ya Mkoa wa Arusha ni shwari hakuna matukio makubwa ya kihalifu.

"Kama ilivyo desturi kote Duniani waumini wa dini ya Kiislam husherehekea sikukuu ya Eid EL-Adh’haa ambapo itasherehekewa kwa siku ya kesho tarehe 21/07/2021"

Kamanda Masejo ameendelea kusema katika kuhakikisha wananchi wanasherehekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu,"Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limejipanga vyema kuhakikisha sikukuu hiyo inasheherehekewa kwa amani nautulivu,kwa kuimarisha doria za miguu na magari"

Ametoa wito kwa wakazi wa Jiji la Arusha na Mkoa mzima wa Arusha kusherehekea kwa amani na utulivu pia kuzingatia tahadhari zote za kiusalama kwa familia pamoja mali zao.Pia kwa watumiaji wa Barabara wafuate sheria taratibu na kanuni za usalama Barabarani ikiwa ni pamoja na watembea kwa miguu na watumiaji Kwa vyombo vya moto wasiendeshe magari hayo wakiwa wamelewa

" Mwisho Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linawatikia wananchi wote Sikukuu njema ya Eid EL-Adh’haa".

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishina msaidizi wa Polisi ACP JUSTINE MASEJO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...