Na Mwamvua Mwinyi, MAFIA
WAZIRI
wa ardhi ,nyumba na maendeleo ya makazi ,William Lukuvi ameiagiza
halmashauri ya wilaya ya Mafia kuchangamkia fursa ya uwekezaji kwani
Mafia ni kisiwa chenye fukwe nzuri inayohitaji wawekezaji wakubwa katika
sekta ya utalii .
Lukuvi
aliyaeleza hayo katika kijiji cha Gonga ,wakati wa ziara yake ya
kutatua kero za ardhi kwenye wilaya mbalimbali mkoani Pwani ,akitangaza
Kampeni maalum "TOKOMEZA KERO " ambapo alipata fursa ya kujionea fukwe
za bahari ambazo hazina mkakati mahsusi wa kuvutia wawekezaji wakubwa
kwenye sekta ya utalii .
"Nasisitiza
hakuna budi mkachangamkia fursa hii na mhakikishe mnaifanyia kazi kwa
maslahi ya wilaya ,mkoa na Taifa kuongeza pato na kuinua uchumi "
"Sikutarajia
kukuta vivutio vizuri hivi wilayani hapa ,hasa katika upande wa fukwe
ambazo zimeambaa eneo kubwa la kisiwa pamoja na ardhi ambayo ni kubwa na
ikipangwa kimkakati itakaribisha wawekezaji wengi kuwekeza kisiwa hiki
tulivu "alifafanua Lukuvi .
Pia
,amekagua mashamba makubwa yanayolalamikiwa katika kijiji cha Gonga
kwenye mashamba ya Utumaini ekari 4,040 na Kigomani ekari 670 ambayo
mmiliki wake yuko hatua za kupata wabia wa kuwekeza .
Lukuvi
baada ya kusikiliza pande zote zinazohusika na mgogoro huo akaelekeza
halmashauri kupitia nyaraka za umiliki wa maeneo hayo kwa umakini kabla
ya kumshauri hatua za kuchukua .
Mkuu
wa wilaya ya Mafia ,mhandisi Martin Ntemo alisema kumekuwa na migogoro
ya muda mrefu ya ardhi iliyohusu zaidi maeneo makubwa yanayomilikiwa na
watu ama kampuni binafsi yakiwa katika mgogoro na wananchi wanaoishi
katika vijiji jirani na maeneo hayo .
Kisiwa
cha Mafia ni kisiwa cha tatu kwa ukubwa nchini kikiunda moja ya wilaya
saba za mkoa ,kina ukubwa wa kilometa za mraba 972 ambazo kati yake
kilometa za mraba 407 ni nchi kavu na kilometa za mraba 565 ni enei la
maji ,kuna wakazi 53,083 ambao wanajishughulisha na shughuli za utalii .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...