*Wabainisha namna nchi itavyonufaika na uwekezaji katika sketa hiyo.

Na Chalila Kibuda ,Michuzi TV Mamlaka   ya Udhibiti  wa Mkondo wa Juu wa Petroli(PURA),imesema kuwa hadi sasa Mamlaka yao imeingia mikataba takribani ya Kampuni 11 kati ya hizo ni Kampuni Tatu zipo katika  uzalishaji wa mafuta na gesi asilia.

Akizungumza jana mkoani Dar es Salaam,katika maonesho ya 45 ya biashara ya kimataifa sabasaba, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Mhandisi  Charles  Sangweni
 amesema mwaka  2010,PURA ilifikia hadi kampuni  27 lakini ilipofika mwaka 2014 bei ya mafuta ilishuka sana  huku kampuni nyingi ziliondoka.

Sangweni amesema katika kampuni hizo 11ni kampuni moja ni la wazawa wa ya kitanzania ambao yanawekeza katika uzalishaji wa sekta hiyo ya mafuta na gesi asilia.

Amesema  kila mkataba unaoingia na PURA,ni lazima TPDC iipitie kwani  ni mbia hivyo uzawa wao unadhibitisha kupitia TPDC,

"Pamoja na hayo tunachokifanya kwetu  , Makampuni yaliyopo katika mikataba sio watekelezaji wa shughuli zote  za utafutaji  wa mafuta na gesi asilia kwahiyo zipo  kampuni nyingine  zinazoshiriki kuchimba kwenye kulisha wachimbaji,Ulinzi,Usafiri,Mawasiliano  na hayo yote ni Kampuni za  kitanzania,"amesema Sangweni.

Amesema fursa zilizopo katika tasnia hiyo ya  Mkondo wa juu zinasimamia kupitia sheria ,Miongozo na kanuni,  lakini vyote hivyo havitoshi  katika usimamizi hadi kuonana na watu wanaosimamia na shughuli hizo ili kuwapa maelezo ya kina juu ya shughuli wanazozifanya na Mamlaka hiyo.

"Kupitia maonesho haya  tutawapa maelezo mazuri namna gani anaweza akaja na akatuona au kuingia katika mitandao yetu ili ajue fursa gani ambazo anaweza wakachukua,"alisema na kuongeza

"Hapa nchini kuna rasiliamali nyingi  katika shughuli ya utafutaji na mambo  mengi  hivyo kuna fursa mbalimbali za Ajiira,Chakula,Usafirishaji hivyo  hata mtu akiwa mwenyewe anaweza akapata nafasi katika kupata fursa,"alisema

Amesema mwekezaji akiingiza mtaji wake mara baada ya kumaliza na kuanza uzalishaji  kinachofuata ni kufanya mgawanyo wa faida na Pura kutokana na kile kilichowekezwa.

Amesema Rasilimali ya mafuta na Gesi asilia lazima zilete faida kwani usimamizi huo ndio utafanya faida kuweza kupatikana.

Naibu Waziri wa Nishati Stephen Byabato akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) Mhandisi Charles Sangweni wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea Banda la PURA katika maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Nishati Stephen Byabato akipata maelezo namna vitu vinavyofanyika katika michoro kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PURA wakati Naibu huyo alipotembelea Banda la Pura  katika maonesho ya Sabasaba.
Mkuu wa Kitengo cha Ushirikishaji wa Wazawa na Ujumuishaji wa Wadau wa  Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) Charles Nyangi akizungumza na waandishi Habari kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka hiyo kwenye maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba)jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti ya Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) Mhandisi Charles Sangweni akizungumza na waandishi wa Habari  kuhusiana na kazi ya PURA katika Maonesho ya Sabasaba

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...