Na Yeremias  Ngerangera, Namtumbo

Naibu waziri wa kilimo ushirika na umwagiliaji  Husein Bashe aliyasema hayo wakati wa kukagua mashamba ya NAFCO ( National Agriculture and food cooperation ) nyumba za wafanyakazi zilizotelekezwa  pamoja na kukagua kituo cha utafiti cha uyole kilichopo  kijiji cha suruti  wilayani Namtumbo ambacho nacho hakifanyi kazi na kusema kuwa mwache Mwalimu Nyerere aitwe baba wa taifa .

Bashe  alionesha kusononeshwa na Juhudi zilizofanywa na mwalimu wakati wa utawala wake wa kutaka kuimarisha kilimo na  kuanzisha mashamba ya NAFCO Pamoja na kuanzisha kituo cha utafiti cha mbegu katika kijiji cha Suruti alidai jitihada hizo lazima zienziwe kwa kuhakikisha kituo cha utafiti  hicho kinafanya kazi kama kilichokusudiwa pamoja na kuhakikisha mashamba ya NAFCO yanalimwa kama lengo lilivyokusudiwa .

Bashe  alikagua Ghala kubwa la NAFCO ,mashamba hekta 6000  kukagua nyumba zilizokuwa zinatumiwa na wafanyakazi ni nyumba 17 huku  katika kituo cha utafiti pia alikagua mashamba hekta 388 na nyumba 16 zilizokuwa zinatumiwa na watumishi wa kituo wakati kituo kinafanya kazi.

Matenus Kapinga mwangalizi wa shamba na nyumba za NAFCO alisema kuwa kazi yake kubwa ni kukodisha mashamba na kiasi cha fedha kinachopatikana kinaingizwa katika akaunti ya wizara ya fedha kwa kuwa wizara ya fedha ndiye mmiliki wa mashamba hayo.

Generosa  Kayombo mkulima katika mashamba ya NAFCO alifikisha malalamiko ya wakulima kwa Naibu waziri wakilalamikia bei ya pembejeo  za mbolea lakini pia wakalalamikia bei ndogo ya mazao ya mkulima akitolea mfano wa zao la mahindi ambalo kwa sasa bei ya soko kilo ni shilingi 220.

Katika ziara hiyo pia Naibu waziri alikagua ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha vifungashio na kusikiliza kero kutoka kwa meneja wa chama kikuu cha ushirika  Juma  Mwanga ya kutonunuliwa kwa tumbaku tani 200  ambapo pamoja na mambo mengine waziri alikipongeza chama kikuu SONAMCU kwa kutumia mapato yao ya ndani kujenga kiwanda hicho lakini akaahidi kuongea na makampuni yanayonunua tumbaku ili kuimalizia tumbaku tani 200 za wakulima zilizobaki alisema Bashe.

Ziara ya waziri wa kilimo wilayani Namtumbo imetoa majibu kwa viongozi wa wilaya kujibu malalamiko ya wananchi waliokuwa wanahitaji kurejeshewa mashamba ya NAFCO na yale ya chuo cha utafiti Suruti yarudishwe kwa wananchi ili waweze kugawiwa kutokana na mashamba hayo kutelekezwa na kutofanya kazi iliyokusudiwa  Bashe  amewahakikishia  viongozi wa wilaya kuwa serikali  kwa sasa itahakikisha mashamba hayo  yanafanyakazi kama ilivyokusudiwa kuanzia sasa.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...