Na Munir Shemweta, SUMBAWANGA
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
amezindua mradi wa nyumba 20 za makazi za Jangwani zilizopo katika
manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa.
Uzinduzi
wa nyumba hizo uliogharimu bilioni 1.6 umefanyika leo tarehe 19 Julai
2021 katika manispaa ya Sumbawanga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali
wakiwemo wakuu wa wilaya za mkoa wa Rukwa, wabunge, madiwani na
viongozi wa chama.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa nyumba hizo, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Mabula alisema, uhitaji wa nyumba nchini bado ni
mkubwa lakini uwezo wa shirika la NHC peke ni mdogo ingawa kwa sasa
kasi ya shirika ni kubwa katika kuendesha miradi mbalimbali.
Alisema,
Wizara ya Ardhi iko tayari kuhakikisha inalifutailia shirika la Nyumba
la Taifa ili liweze kutekekeza majukumu yake kama lilivyoaminiwa na mhe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa
mujibu wa Dkt Mabula, NHC ni shirika pekee la umma ambalo halipati
ruzuku ya kuendesha miradi yake na kukielezea kitendo hicho cha kutopewa
ruzuku kama kinalifanya shirika kuhitaji na miradi mingi ili liweze
kujiendesha kibiashara.
Aliushukuru
uongozi wa halmashauri ya manispaa ya sumbawanga kwa uamuzi wa
kuwapangishia watumishi wake katika nyumba za NHC zilizozinduliwa na
kuuelezea uamuzi huo kama motisha kwa watumishi
"
kitendo cha kuwapangishia nyumba watumishi ni cha kijasiri na
kinamfanya mtumishi asiwe na sababu ya kutokuja manispaa ya Sumbawanga
kwa kuwa ana uhakika wa makazi na atafanya kazi kwa weledi" alisema Dkt
Mabula.
Kwa upande wake
Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini Aeshi Hilali alisema, pamoja na
kutekelezwa na kukamilika kwa mradi wa nyumba za NHC Jangwani lakini
Sumbawanga bado ina changamoto ya ujenzi wa hospitali ya wilaya
aliyoieleza iko nje ya mji.
Aliomba
maeneo yanayotoa huduma kwa wananchi yaliyoko nje ya mji ni vizuri
maeneo hayo yakapewa kipaumbele kwa kupatiwa miradi ya majengo ya makazi
ili watumishi watakaofanya kazi maeneo hayo waweze kupanga na kufanya
kazi kwa ufanisi.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
akizindua mradi wa nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa ( NHC) za
Jangwani zilizopo halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa leo
tarehe 19 Julai 2021
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...