Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akipiga bastola juu kuashiria Uzinduzi wa mashindano ya Kimataifa ya Riadha (Zanzibar International Marathon) ya kilomita 21 zilizoanzia leo katika viwanja vya Ngome Kongwe Mjimkongwe na kumalizia katika Uwanja wa Amaan Studium Jijini Zanzibar.[Picha na Ikulu] 18/07/2021.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akimkabidhi shada la
mauwa Nd,Pamela Chepkoech kutoka Nchini Kenya akiwa mshindi wa kwanza
Wanawake katika mashindano ya Kimataifa ya Riadha (Zanzibar
International Marathon) ya kilomita 21 alietumia Saa 1:19:50
yaliyofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium Jijini
Zanzibar.[Picha na Ikulu] 18/07/2021.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akimvalisha nishani
Nd,Panuel Mkumbo kutoka Nchini Kenya akiwa mshindi wa kwanza Wanaume
katika mashindano ya Kimataifa ya Riadha (Zanzibar International
Marathon) ya kilomita 21 aliyetumia Saa 1:04:48 yaliyofanyika leo
katika Uwanja wa Amaan Studium Jijini Zanzibar.[Picha na Ikulu]
18/07/2021.
Wanariadha katika mashindano ya Kimataifa ya Riadha (Zanzibar International Marathon) ya kilomita 21 wakijitayarisha kuanza Mbio hizo leo katika Uwanja wa Amaan Studium Jijini Zanzibar,ambapo mgeni rasmin alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi(hayupo pichani).[Picha na Ikulu] 18/07/2021.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...