Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amewataka Watumishi wote wanaokwenda kutekeleza na kuhakiki Kaya maskini kuhakikisha wanazingatia Weledi ili Mradi wa TASAF Kipindi Cha pili cha awamu ya Tatu kiweze kuwa na mafanikio makubwa Katika kupiga Vita Umaskini.

RC Makalla amesema hayo wakati wa Ufunguzi wa Semina ya kuwajengea uelewa Viongozi, Watendaji na wawezeshaji wa TASAF Wilaya ya Ilala ambapo amesema lengo la awamu hii ya Tatu ni kufikia asilimia 100.

Aidha RC Makalla amesema kumekuwa na kamchezo ka watu kuingiza majina ya watu ambao sio walengwa na kuacha wale walengwa wakitaabika Jambo ambalo ni kinyume na malengo ya Serikali hivyo ni vyema awamu hii wakahakikisha kasoro hizo Hazijirudii.

Hata hivyo RC Makalla ametoa wito kwa Walengwa watakaopata fedha hizo kuhakikisha wanazitumia vizuri kwa kuanzisha miradi ya ujasiriamali itakayowakwamua kiuchumi huku akiwataka Madiwani kushiriki Katika kusimamia fedha hizo ili zifike kwa wahusika 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...