Charles James, Michuzi TV

SERIKALI imetangaza kuwa tayari mchakato wa kuingiza na kutoa chanjo ya ugonjwa COVID-19 (Corona) umekamilika huku ikisisitiza tahadhari zaidi ziendelee kuchukuliwa na wananchi.

Kauli hiyo imetolewa leo Julai 4,2021  jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Profesa Abel Makubi kwenye mkutano wake na wandishi wa habari ambapo amesisitiza kuwa chanjo hiyo ni hiari.

Prof. Makubi amesema Serikali itatoa chanjo hiyo bure bila kuwatoza wananchi huku akionya kuwa hawataruhusu uingizwaji holela wa chanjo hiyo au kutoza fedha kwa ajili ya kuchoma chanjo hiyo.

Amesisitiza ofisi zote za serikalini nchini wananchi wanaoenda wakiwemo watumishi na kuzingatia taratibu zote za kitabibu za kujikinga na ugonjwa huo ikiwemo kuvaa barakoa kabla ya kuingia kwenye Ofisi hizo pamoja na kuwepo kwa maji tiririka kwa ajili ya kunawa mikono.

" Tunatoa ushauri kwa Ofisi zote za Umma nchini kuzingatia taratibu za kujikinga na Corona kwa kuweka vifaa vya maji tiririka ili kila mwananchi anaeingia aweze kunawa mikono lakini pia tunasisitiza uvaaji wa Barakoa," Amesema Prof Makubi.

Aidha Prof. Makubi amesema miongozo na utaratibu huo ufuatwe pia mashuleni kwa kuhakikisha kunakua na Maji tiririka na uvaaji wa barakoa.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Profesa Abel Makubi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...