Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
Michuano ya Vijana ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Challenge Cup 2021) imehitimishwa nchini Ethiopia kwa Timu ya Taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka 23 kutwaa Ubingwa huo baada ya ushindi wa jumla ya Mikwaju ya Penalti 6-5 dhidi ya Timu ya Taifa ya Burundi.
Mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Bahir Dar nchini Ethiopia, Tanzania na Burundi zilitoka sare ya 0-0 katika dakika 90 za mchezo huo wa kukata na shoka kwa pande zote mbili.
Hali ya kutoka sare katika dakika zote 90 ni baada ya ubora wa timu zote mbili katika mchezo huo wa Fainali uliowakutanisha nchi hizo mbili za Afrika Mashariki. Mikwaju ya Penalti iliamua Ubingwa wa Tanzania katika Michuano hiyo.
Tanzania U23 ilifuzu Fainali ya Michuano baada ya kuifunga Sudan Kusini bao 1-0 katika dakika 90 za mchezo huo wakati Burundi walifuzu Fainali hiyo baada ya ushindi wa Penalti dhidi ya Kenya.
Timu ya Taifa ya Sudan Kusini wameibuka kuwa Washindi wa tatu wa Michuano hiyo baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kenya katika mchezo wa (Play-Off) kutafuta Mshindi wa tatu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...