Na Zainab Nyamka, Michuzi TV
Kwa sasa
Dawasa inatoa huduma kwa asilimia 92 kwa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani
na wakitumia takribani Bilioni 50.4 kwa mwaka katika kuboresha huduma za
maji.
Waziri wa Maji
Jumaa Aweso ameweza kuzindua Cheti cha Ubora ISO na magari ya kutolea
majitaka yatakayotumika kuboresha huduma ya majitaka ndani ya Jiji la
Dar es Salaam.
Hayo
yamesemwa wakati wa hafla iliyoandaliwa na Mamlaka hiyo leo Jijini Dar
es Salaam na kuhudhuriwa na wabunge wa Mikoa inayohudumiwa nayo na
kuwashukuru Dawasa kwa kufanikisha miradi mikubwa na kuondoa changamoto
ya maji kwenye maeneo yaliyokuwa hayana huduma.
Akizungumza
wakati wa hafla hiyo, Mbunge wa Ilala Mussa Zungu amempongeza Afisa
Mtendaji Mkuu wa Dawasa Cyprian Luhemeja kwa kuisimamia vizuri Mamlaka
hiyo na kufikia malengo waliyojiwekea na
Zungu
amesema, Kwa upande wa Wilaya ya Ilala changamoto kubwa ni upande wa
majitaka ambapo ameona leo uzinduzi wa magari ya majitaka na hilo
linaenda kuchagiza uboreshaji wa huduma ya majitaka na amemsikia
Mhandisi Luhemeja akielezea mkakati wa ujenzi wa miradi mikubwa ya
majitaka.
Mbunge wa Jimbo
la Ukonga Jerry Silaa, amemshukuru mtendaji mkuu pamoja na watendaji
wote wa Dawasa kwa kufanikisha maji kufika katika jimbo lake ikiwa ni
miaka mingi wakiwa hawapati majisafi na Salama.
Silaa
amesema, watendaji wote wanafanya kazi kubwa sana na wananchi wa Ukonga
wanapata maji yakiwa yamefika kwa uhakika wakitumia tanki la Pugu
ambalo lilizinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia
Hassan Suluhu.
Naye
Mbunge wa Segerea, Bonna Kamoli amesema dawasa wanatenda haki ushahidi
huo anao kwa sababu katika Jimbo lake hakukuwa na maji ila sasa wananchi
wake wameanza kupata maji safi na miradi mingine ya kimkakati
ikiendelea kujengwa.
Wabunge
wengine waliohudhuria ni Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete, Hawa
Mchafu, Subira Mgalu, Abdalla Chaurembo, Mbunge wa Kibamba Mtevu na
Mbunge wa Bagamoyo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa
Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akipokea tuzo
kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya DAWASA Jenerali Mstaafu
Davis Mwamunyange wakati w hafla ya tathmini ya utendaji kazi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...