Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
Wakazi wa Kigamboni na Mkuranga kuondokana na kero ya maji mara baada ya kumalizika unategemea kukamilika mwaka 2022. Hii ni kutokana na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) kutenga fedha kwa ajili ya miradi hiyo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mara ya kumaliza ziara hiyo, Naibu Waziri, Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema serikali iko makini hasa kwenye kusimamia miradi ya maji ili kuondoa changamoto ya upatikanaji wa maji katika maeneo mbalimbali ya hapa nchini.
Pia amempongeza Afisa Mtendaji Mkuu, Cyprian Luhemeja kwa kuwapa nafasi wafanyakazi waliochini yake ili kuonesha uwezo mkubwa wa kazi na hii inajidhiirisha kwamba wameweza kuonesha umahili hasa kwenye kusimamia miradi mbalimbali ya DAWASA ambayo ni mikubwa kwa kushirikisha wataalamu wa ndani wakiwemo wa Wizara ya Maji pamoja na na wakandarasi wageni ili kupelekea kupata ujuzi zaidi.
Amesema kutokana na kutumia wataalam wa ndani hasa wakandarasi wataweza kubaki na ujuzi hivyo wataweza kusimamia miradi mingine inayokuja ili kuwainua zaidi na kupelekea kupunguza gharama kwa kutumia wakandarasi wazawa ili kuweza kuwafikishia huduma ya maji wananchi.
Pia amewapongeza DAWASA kwa kutoa nafasi kubwa kwa wanawake na kupelea kufanikisha miradi mbalimbali hivyo ametoa wito kwa taasisi mbalimbali kuiga mfano wa Mamlaka hiyo kuwaamini wanawake kwani wanaweza kufanya kazi kiufanisi na bila shida yoyote maana hawahitaji kuona mwanamke anapendelewa ila apimwe uwezo wake ili kuwa na wataalam wazuri.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Miundombinu na Uwekezaji DAWASA, Mhandisi Ramadhani Mtindasi mradi wa Kisarawe II utakaosaidia kuondoa kero ya Maji katika Kata saba za wilaya ya Kigamboni kutokana na kuchimba visima katika eneo la Kigamboni na kujenga tenki la maji litakalokuwa linaweza kuhifadhi maji lita Milioni 15.
Pia amesema Mradi wa Mkuranga – Vikindu umeweza kupunguza kero ya maji hasa maeneo ya Mkuranga hivyo mradi huo ukimalizika utaweza kuondoakero ya maji mara baada ya kujenga tanki la maji linalohifadhi maji lita milioni 1.5.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...