Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Damas Ndumbaro amezindua Utalii wa Faru katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi iliyopo Wilayani Same, Kilimanjaro. Uzinduzi huo umeshuhudiwa na Naibu Waziri wa Maliasili, Mary Masanja, RC wa Tanga, Adam Malima na DC wa Same, Edward Mpogolo.

Waziri Dk Ndumbaro amesema Hifadhi ya Mkomazi ni muhimu ingawa ina changamoto ya upatikanaji wa maji kwa ajili ya wanyama na binadamu ambapo ameziagiza Mamlaka zinazohusika kuhakikisha mabwawa yanachimbwa mara moja ili wanyama wasiende umbali mrefu kutafuta maji.

Dk Ndumbaro pia ameielekeza mamlaka ya wanyamapori kuhamisha baadhi ya Nyumbu waliopo kwenye Hifadhi ya Serengeti kuletwa Mkomazi ili kukidhi haja ya wageni kwani kwa sasa Mkomazi haina aina hiyo ya wanyama.

" Tunataka kuongeza idadi ya watalii kufika Milioni 5 ifikapo mwaka 2025 na kupata mapato yatokanayo na utalii kiasi cha Sh Bilioni 6 kutoka kiasi cha Sh Bilioni 2.6 kwa sasa,"Amesema Dk Ndumbaro.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Same, Edward Mpogolo ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu Utalii huo huku akisema anaamini utachochea ukuaji wa uchumi wa Same.

"Nimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu Faru hawa kutumika kwa Utalii kwenye Hifadhi ya Mkomazi, kwa kuruhusu Utalii wa Faru kutaongeza Watalii na Mapato kwa Serikali, Niwaombe Wananchi wa Same kuchangamkia fursa hiyo kwa kujenga Hoteli nzuri," Amesema DC Mpogolo.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...