
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii , Mhe. Mary Masanja (Mb) akimsikiliza Mhifadhi Mkuu, Hifadhi ya Mazingira Asilia Rondo, Richard Baltazar (kulia) akitoa maelezo kuhusu Hifadhi ya Mazingira Asilia Rondo alipokuwa akikagua shamba la miti Rondo katika ziara yake ya kikazi leo Mkoani Lindi.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii , Mhe. Mary Masanja (Mb) akimwagilia mti wa kumbukumbu alioupanda wakati wa ziara yake ya kikazi katika Ofisi za Wakala wa Huduma za Miti (TFS) Shamba la Miti Rondo leo Mkoani Lindi. Kushoto ni Mkuu wa Kanda ya Kusini wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Manyisye Mpokigwe

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii , Mhe. Mary Masanja (Mb) akizungumza na wanachi wa Kijiji cha Rondo katika Halmashauri ya Wilaya ya Lindi katika ziara yake ya kikazi ya kusikiliza kero za wananchi ambapo amewataka wananchi kuendelea kuhifadhi mazingira ili kuendeleza utalii wa eneo hilo Mkoani Lindi leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...