Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
KIUNGO Mkabaji wa Kimataifa wa Uganda, Khalid Aucho rasmi amesaini kandarasi ya miaka miwili na Klabu ya Yanga baada timu hiyo kushinda vita ya usajili na Watani wao Simba SC katika kupata saini ya Kiungo huo.

Yanga SC wamekamilisha usajili wa Aucho mapema leo Agosti 9, 2021 huku dili hilo lilkishuhudiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Klabu hiyo, Haji Mfikirwa. Imeelezwa kuwa Aucho alikuwa anawindwa na Klabu nyingi katika usajili wake hadi Yanga SC kunasa saini yake.

“Sisi kama Yanga SC tumefanya usajili wa Mchezaji huyo mwenye CV nzuri na naamini atatusaidia. Usajili huu ni pendekezo la Kocha Nabi wakati anaenda mapumziko aliacha maelekezo ya kusajili Wachezaji kama hawa ambao tunawasajili sasa”, amesema Mfikirwa.

Amesema hadi kukamilisha dili hilo la uhamisho la Aucho, Klabu yao imefanya ushawishi mkubwa kwa Mchezaji huyo hadi kupata saini yake akitokea katika ya Makkasa SC ya nchini Misri.

“Haikuwa kazi nyepesi, Khalid Aucho alikuwa na ofa nyingi sana, hadi tunamsajili tumefanya ushawishi mkubwa na sio jambo dogo na tunafurahi kufanikisha jambo hili”, ameeleza Mfikirwa.

Kwa upande wake, Mchezaji Khalid Aucho amethibitisha hadi kukamilisha usajili huo alifuatwa pia na Klabu ya Simba SC kwa lengo la kumsajili. Aucho amesema Simba SC walizungumza na Wakala wake wakati Yanga SC walimfuata mwenyewe kufanya mazungumzo hayo.

“Simba SC walimfuata Wakala wangu, lakini Yanga SC walinifuta mimi binafsi ili kukamilisha usajili wangu, mimi na Eng. Hersi tulizungumza kama Familia kufanya usajili huu, naamini nitacheza kwa moyo mmoja Yanga SC kama sehemu ya Familia yangu.”Amesema Aucho.
Kiungo Mkabaji wa Kimataifa wa Uganda, Khalid Aucho (wa pili kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM, Eng. Hersi Said baada ya kukamilisha dili la uhamisho la miaka miwili katika Klabu hiyo mapema leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...