Na Said Mwishehe,

KWAKO Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Soka ya Simba yenye makazi yake Mtaa wa Msimbazi katika Jiji la Dar es salaam, Barbara Gonzalez.

Nikiri tangu umekuwa Mtendaji Mkuu, CEO wa Simba sijawahi kuandika chochote kuhusu wewe, sijawahi kueleza chochote, sijawahi kukuzungumzia.Ndio sijawahi kueleza lolote kuhusu Babra.Leo nasema hapana ,acha nieleze kitu kuhusu Barbara.

 Barbara Gonzalez ukweli ni kwamba wewe ni Iron Lady, wewe ni mwanamke wa Shoka, wewe ni mwanamke jasiri, mwanamke wa nguvu na yote kwa yote wewe ni Malkia wa nguvu.

Katika soka la Tanzania wewe ni mwanamke wa mwaka 2021.Uwepo wako ndani ya Simba umekuwa na tija na faida kubwa.Hongera dada wa watu ,unastahili sifa na heshima.

Nikiri wakati unateuliwa kushika nafasi hiyo wapo waliokubeza, wapo waliokuona wewe si lolote si chochote lakini nikwambie kwa utendaji wako ndani ya Simba umeifanya klabu yako kuwa imara kuliko juzi na jana.

Simba imekuwa bora kuliko wakati wowote, Simba imekuwa brand kubwa ndani na nje ya Tanzania. Simba imekuwa na mafanikio makubwa.Umeifanya Simba kuuza wachezaji kwa mabilioni ya fedha🙌.

Najua kuna mwekezaji Mohamed Dewji almaarufu MO ambaye anatoa fedha kufanikisha utendaji wako kuanzia usajili,maandalizi ya timu, ulipaji mishara na posho pamoja na mambo mengine yanayohitahi fedha .

Ukweli utabaki kuwa wewe Barbara una akili nyingi sana na unajua kuzitumia.Wanawake wa aina ya Barbara ni wachache sana hapa duniani na Simba imebahatika kuwa naye.

Kwa utendaji wako uliotukuka ndani ya  Simba naamini jina lako litaandikwa kwa wino wa dhahabu,unastahili heshima hiyo,wapo watakaobeza sijali maana ndio kawaida ya wabongo

Barbara unajua kukabiliana na changamoto kubwa na ndogo zinazojitokeza kwenye Klabu yako .Najua unasimama kwenye uchapakazi na nidhamu.Ni wewe ambaye umewafanya wachezaji wa Simba kujua thamani yao.Umewafanya wachezaji kuwa na nidhamu na hushindwi kuchukua hatua.

Ukitaka ushahidi kumbuka ishu ya Jonas Jerald Mkude, alipozingua kwenye nidhamu ukamwambia haiko hivyo na adhabu juu,leo Mkude amenyooka amekuwa mtamu kama sukari.

Barbara hakuna jambo ambalo amesimamia akashindwa, kila alichosimamia amekifanikisha angalia Simba Super Cup ilifana hatari achilia mbali Simba Day .Mbona raha ..

Naposema hujawahi kushindwa ipo mifano mingi, hata ile filamu ya Haji Manara na tuhuma za kuihujumu Simba bado tunaikumbuka.Barbara ulitumia akili ya kuzaliwa  na ile ya shuleni kubaini hujuma na hatimaye aliyetuhumiwa kuihujumu Simba leo amedhihirisha baada ya kujiunga rasmi Yanga.

Haji Manara baada ya kujua kanasa kwenye mtego wa Barbara akaamua kusema mengi kupitia mitandao ya kijamii, sote tulimsikia, ndio na akaenda mbali zaidi kwa kusema kabla ya yeye(Manara) kuondoka Simba basi Barbara ataondoka yeye.

Iron Lady Barbara akakaa kimya anaangalia rada zake zinasoma wapi.Kwani ilipita siku nyingi Manara akaamua kusalimu amri,akatangaza kuondoka Simba, Barbara akabaki kimya, si unajua tena ukiwa na akili ya kuzaliwa jumlisha na shuleni.

Ukimya wa Barbara ni wazi umeendelea kumtisha Manara na leo ameona isiwe tabu karudisha mpira kwa kipa, amekwenda Yanga.

Wenye akili wanajua kabisa mtoto wa Kariakoo kazidiwa, hana tena ujanja, kaisha kabisa.

Nikiri siwezi kumlaumu Manara kwenda Yanga maana anahistoria nako, baba yake ni mwana Yanga ,amechezea Yanga.Hivyo Haji amerudi nyumbani lakini swali linakuja amerudije rudije?

Jibu ni kwamba amerudi baada ya kukutana na mwanamke wa Shoka,mwanamke ambaye kabla ya kuanika uovu  anakuchunguza na anajiridhisha.

Katika vita ya Barbara  Gonzalezna Haji Manara ni wazi Manara amebakia kuwa mateka anayehitaji huruma kwa wapinzani wa Simba.

Nimalizie kwa kusisitiza Barbara wewe ni hazina ya soka la Tanzania , unajua kusuka mipango,unajua kupambana na adui yako bila kelele.

Nakumbuka wakati Manara analalama kudukuliwa na kutuhumiwa kutoa siri za Simba kwa Yanga...

Barbara  ulipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu yaliyosemwa na Haji Manara,ukajibu kwa kifupi "Nimeona lakini akili yangu nimeelekeza kwenye mechi ya Kigoma kuhakikisha unashinda".

Kuna wakati namuona Barbara  Gonzalez kama mwanamke mwenye kifua cha kiume,kifua chenye kuhimili mambo mazito,kifua kinachoweza kubeba yasiyobebeka.Najua kuna wanaume wenye vifua vya kike, jambo dogo kwao kuuubwa.Wakipitia changamoto kidogo basi kilele mwaka mzima.

Nimeandika weee sasa inatosha, nihitimishe kwa kukusalimia Babra shikamoo.Unastahili kuheshimiwa na wana Simba, hakika wakuheshimu.Ila wee Barbara Gonzalez nomaa sanaa , umemtisha katishika, umemfanya sasa anahaha na amepata mhaho.😂 😂 😂 .

 No; 0713833822

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...