Na Farida Sady, Morogoro
BODI ya Wakurugenzi ya shirika la Ugavi wa umeme Tanzania TANESCO imesema kuwa imeridhishwa na hatua zinazochukuliwa na uongozi wa shirika hilo Mkoani Morogororo ya kurejesha huduma ya umeme kwa hatua za awali.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa bodi hiyo Alexander Kyaruzi mara baada ya kufanya ziara katika katika kituo hicho pamoja na eneo la Tungi ambapo inaamini kuwa ni chanzo cha mlipuko uliosababisha kuungua kwa jengo la la kuthibiti mfumo wa upande wa umeme usongo wa kilovati 33 katika kituo cha kupozea na kusambaza umeme cha Msamvu Mkoani huo august 02,2021.

Aidha bodi hiyo ilipotembea kituo hicho imewataka wananchi kuendelea kuwa na subra wakati shirika hilo likiendelea na juhudi za kupata Umeme kutoka vituo vya jirani ili huduma iweze kurejea katika hali yake

Kwa upande wake Msimamizi wa kituo cha Umeme Cha Msamvu Mhandisi Loserian Joseph Kilusu amesema kuwa mara baada ya kutoea kwa moto huo walichukua hatua za awali za kuizima na baadae ndipo walipooita jeshi la zimamoto na Uokoji kwa msaada zaidi.

Nae Meneja wa Usafirishaji vituo vya kupozea Umeme Nchini Mhandisi Zakaria Mgalama amesema kuwa jukumu lao kubwa kwa sasa ni kuhakisha wanannachi wa Mkoa wa Morogoro wanapata huduma hiyo kama awali.

Meneja wa Usafirishaji vituo vya kupozea Umeme Nchini Mhandisi Zakaria Mgalama akitoa maalezo kwa Bodi ya Tanesco ya namna ya tukio lilivyotokea katika eneo la Tungi Manispaa ya Morogoro ambapo inaaminika kuwa ndio chanzo cha mlipuko katika jengo la la kuthibiti mfumo wa upande wa umeme usongo wa kilovati 33 katika kituo cha kupozea na kusambaza umeme cha Msamvu Mkoani huo august 02,2021.
sehemu ya mitambo iliyoungua katika kituo cha kupozea umeme cha msamvu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...