Na Said Mwishehe,Michuzi TV
KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM,Daniel Chongolo amesema kuwa Chama hicho ni kikubwa kuliko mtu yoyote,hivyo hakuna pembe zaidi na hao wanaaofikiria kushindana wameshaanza kuchukuliwa hatua.
Kauli ya Chongolo inakuja kukiwa na wimbi la kauli kizani zinazotolewa na baadhi ya wanachama wa Chama Chama wakiwemo baadhi ya Wabunge ambao wamekuwa wakitoa kauli mbalimbali zinazokwenda tofauti na msimamo wa Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali yake kuhusu hatua zinazochukuliwa kukabiliana na Janga la Uviko 19 ikiwemo uchomaji wa Chanjo.
Amesema kwamba katika Chama hicho ukiondoka Mwenyekiti,Makamu Mwenyekiti anayefata kwa ukubwa ni nafasi ya Katibu Mkuu lakini bado na yeye hana mamlaka ya kuweka mambo yake kwani Chama kinauwezo wa kumchukulia hatua.
" Hiki ni Chama kikubwa kuliko mtu yeyote hata mimi sina Mamlaka ya kuweka mambo yangu sasa sijui baada kwenye Chama hiki baada ya Mwenyekiti,Makamu Mwenyekiti sidhani kama kuna mtu mwenye pembe zaidi,"amesema na kuongeza
"Chama hiki kina utaratibu wake wa kumuwajibisha mtu yeyote,hata mimi Mtendaji mkuu nikifanya mambo ya hovyo nitawajibishwa ,hivyo mtu yoyote asidhani anaweza kuota pembe kuliko wengine,"alisema
Kuhusu Katiba Mpya
Chongolo amesema hakuna Mwananchi ambaye anayebeba bango la kudai Katiba Mpya zaidi ya wanasiasa ambao wanamasilahi yao binafsi.
Amesema masilahi hayo ambayo yamegawanyika katika sehemu tatu ikiwemo yakutaka Tume Huru ya Uchaguzi, demokrasia na uhuru."Tuambie sisi kwani hatuna uhuru?,"amehoji
Aidha amesema Chama hicho nimetoa maelekezo kwa serikali kupitia Halmashauri mbalimbali pamoja na manispaa kuhakikisha zinajenga madarasa na kuboresha miundombinu ya elimu kli wanafunzi waanze masomo kwa wakati.
Amesema kumekuwa na utaratibu wa kucheleweshwa ujenzi wa madarasa na hivyo wanafunzi kushindwa kuanza masomo kwa wakati jambo ambalo kwa sasa Chama hicho hanitaki kuona hali hiyo ilitokea.
"Utoaji elimu bila malipo liwe na tija zaidi ni lazima kuwe na miundombinu rafiki kwa wanafunzi, kwamba wanafunzi wanapoandikishwa waikute miundombinu yote ya kujifunzia inakuwa tayari" amesema na kuongeza
"Suala la miundombinu ya kujifunzia ikiwemo madarasa, madawati,fedha zake zitatolewa katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha, lengo ni kuondoa usumbufu wa kukimbizana na watendaji hata kufikia hatua ya kuzuia likizo zao. Changamoto hii tunataka kuimaliza mapema"Daniel Chongolo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...