Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Halima Bulembo amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM kwa mwaka 2020 - 2025 kwa kipindi cha Januari hadi juni 2021.
Akiwasilisha taarifa hiyo mbele ya wajumbe wa Halimashauri Kuu ya CCM wilayani Muheza ,Bulembo Alisema mojawapo ya mafanikio ni utoaji wa mikopo kwa vijana,wanawake na watu wenye ulemavu isiyo na riba kutokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri.
Jumla ya vikundi 55 vimepata mikopo yenye thamani ya shilingi million 337,000,000.
Vikundi vya vijana vimepata sh .152,000,000/= wanawake sh .152,000,000 na watu wenye ulemavu 33 wamenufaika.
Pamoja na mikopo hiyo mafunzo ya stadi za ujadsiriamali yametolewa na vijana 276,wanawake 324 na watu wenye ulemavu 33 kutoka katika 20 na shughuli za kiuchumi167za vijana,wanawake na makundi emengine zimerasimishwa.
Aidha wajasiriamali 473 wamewezeshwa kukuza uzalishaji na mitaji.
Mikopo hii imeweza kuzalisha fursa za ajira 473 kwa wanawake ,vijana na watu wenye ulemavu.
Home
SIASA
DC Muheza awasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya ccm,aeleza walivyofanikiwa utoaji mikopo kwa kada mbalimbali
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...